In Summary
  • Maribe alieleza wanahabari nje ya mahakama Milimani kwamba hakuwa na mengi ya kusema. 
  • Maribe aliachiliwa Ijumaa juu ya ukosefu wa ushahidi.
Jackie Maribe akiwa katika Mahakama ya Milimani, mbele ya Hakimu Grace Nzioka mnamo Februari 9, 2024, wakati wa hukumu ya kesi ya mauaji ya mfanyabiashara Monica Kimani .
Image: DOUGLAS OKIDDY

Mwanahabari Jacque Maribe amevunja kimya baada ya hakimu Grace Nzioka kumuondolea mashtaka ya mauaji ya Monica Kimani.

Maribe alieleza wanahabari nje ya mahakama Milimani kwamba hakuwa na mengi ya kusema. Hata hivyo alihimiza watu kuenda kusoma kitabu cha Yohana 8:32.

"Sihitaji kusema chochote lakini nitasema nenda kasome Yohana 8:32. Kwa maana mtafahamu kweli na hiyo kweli itawaweka huru. Asante," Maribe alisema.

Mtangazaji  wa zamani wa Citizen, Jacque amekua ndani na nje ya mahakama kwa miaka 5 iliyopita. Alikuwa mshtakiwa wa pili kwa kesi hiyo pamoja na mshtakiwa wa pili, Jowie Irungu.

Mwili wa Monica ulipatikana nyumbani mwake, Lamuria Gardens Apartment ambayo iko kando ya barabara ya Kitale, off Dennis Pritt, Kilimani.

Hata hivyo Maribe aliachiliwa Ijumaa juu ya ukosefu wa ushahidi. Katika hukumu yake, Hakimu Grace Nzioka alisema kuwa mashtaka dhidi ya Maribe haiukuwekwa vizuri.

"Ni maoni yangu kwamba shtaka lililoletwa dhidi ya mshtakiwa wa pili halikuwa shitaka sahihi", hakimu alisema.

" Matokeo yake ni kwamba upande wa mashtaka haukutoa ushahidi wa kutosha kwa mahakama yake kumpata mshtakiwa wa pili na hatia  ya kosa hilo. mauaji ya Monica Nyawira Kimani usiku wa Septemba 19,2018".

Jowie na Jacque wamekua kwenye kesi kuanzia 2018 na upande wa mashtaka kuita mashaidi 35.

Hakimu Nzioka amepata Jowie Irungu na hatia ya kuua Monica Kimani.

View Comments