In Summary

•Mahakama zote nchini kuadhimisha siku ya maombolezi baada ya kifo cha jaji Monica Kivuti hii ni kufutia tangazo la jaji mkuu,Martha Koome.

•Monica alifariki kutokana na majeraha ya risasi baada ya kupigwa na afisa wa polisi kwenye mahakama ya Makadara.

 

Monica Kivuti
Image: Facebook

Mahakama zote nchini Kenya zinaadhimisha siku ya kitaifa ya maombolezo  ya hakimu mwandamizi Monica Kivuti aliyepigwa risasi wakati wa kikao cha mahakama jijini Nairobi.

Kivuti alifariki kutokana na majeraha ya risasi yaliyosababishwa na afisa wa polisi mnamo tarehe 13 Juni 2024 katika Mahakama ya sheria ya Makadara.

Jaji mkuu Martha Koome  ametoa tangazo kuwa kila mahakama sharti iidhinishe  huku akitoa wito kwa wakenya kujitokeza  katika kituo chao cha karibu cha mahakama ili kuadhimisha siku ya kitaifa ya maombolezi kwa jaji huyo.

"Mhe. Kivuti alikuwa afisa shupavu ambaye alikufa akilinda utawala wa sheria... njia bora zaidi tunaweza kuheshimu ahadi yake ni kuendelea kutoa huduma kwa kuzingatia Katiba na sheria,”  taarifa kutoka  kwa Martha Koome ilisomeka.

Vile vile vikao vya mahakama kote nchini vitaendelea  na hali hiyo ya kumpa heshima za mwisho kwa Monica Kivuti,Jumatano isipokuwa mahakama ya sheria ya Makadara ambayo inaendelea kutathminiwa kwa minajili ya usalama.

“Kwa hiyo, mahakama nchini kote zitaendelea na shughuli zake siku ya Jumatano, tarehe 19; Alhamisi, tarehe 20; na Ijumaa, tarehe 21; isipokuwa mahakama za sheria za Makadara, ambazo ziko chini ya kutathminiwa upya kwa madhumuni ya usalama..." Koome alisema

 Aidha,Koome alisema kuwa majaji, maafisa wa mahakama, na wafanyakazi watahitajika kutumia mahakama za mtandaoni  kwenye mahakama za sheria za Makadara.

Hata hivyo,majaji pamoja na mahakimu wameshikilia kuwa hawatafanya kazi kuanzia Jumatano hadi Ijumaa wakidai kupinga ‘mazingira duni ya kazi’.

View Comments