In Summary

• Lenolkulal alipatikana na hatia ya kupokea Sh84 milioni kwa ufisadi kwa usambazaji wa bidhaa za petroli katika serikali ya kaunti alipokuwa gavana.

LWENOLKULAL

Aliyekuwa Gavana wa Samburu Moses Lenolkulal anatarajiwa kusomewa hukumu yake leo hii mahakamani baada ya kupatikana na hatia ya ufisadi Jumatano.

Lenolkulal alipatikana na hatia ya kupokea Sh84 milioni kwa ufisadi kwa usambazaji wa bidhaa za petroli katika serikali ya kaunti alipokuwa gavana.

Hakimu wa kesi Thomas Nzyoki alisema kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani na ODPP, hakuna shaka kuwa Lenolkulal na wakala wake Hesbon Ndathi ndio waliofaidika zaidi na pesa hizo za umma.

Alisema kuna ushahidi mwingi kwamba Lenolkulal akiwa gavana wa Samburu wakati makosa hayo yanasemekana kufanywa yalitenda katika mgongano wa kimaslahi.

Hakimu alitegemea zaidi ya vocha 200 za malipo na lpo kama ushahidi wa biashara ya moja kwa moja ya Lenolkulal na kaunti.

Alisema uadilifu wake uliathiriwa na maslahi binafsi.

"Maafisa wa umma lazima wawe na nia ya dhati katika masuala ya afisi yake. Wanafaa kuzingatia kanuni za utawala bora kila wakati. Kisheria gavana haruhusiwi kufanya biashara na serikali ya kaunti yake," alisema Nzyuki.

Pia alimkashifu katibu wa kaunti ambaye alikuwa mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo kwa jukumu alilotekeleza lililopelekea kupotea kwa theoniew.

Alisema katibu wa kaunti alitia saini na kuidhinisha malipo huku akifahamu kuwa Lenolkulal ndiye mmiliki wa kituo cha huduma cha Oryx.

"Ofisi ya uhasibu ilidanganya kabisa kwa kiapo kwamba hawakujua Lenolkulal ndiye mmiliki wa Oryx. Hawakupaswa kuidhinisha malipo hayo kwa Oryx," ilisema mahakama.

Hakimu alisema ushahidi uliotolewa niko mahakamani na DPP akiongozwa na wakili wa mashtaka Wesley Namache ulikuwa mwingi kwa kuwa washtakiwa wenza wa Lenolkulal walitumia maafisa wao kuidhinisha malipo kwa Oryx isivyofaa.

Lenolkulal alishtakiwa mwaka 2019 kwa matumizi mabaya ya ofisi na mgongano wa kimaslahi na kusababisha hasara ya sh 84milioni.

Ameshtakiwa kwa kutumia kampuni yake ya Oryx Service Station kusambaza petroli na dizeli katika kaunti hiyo.

 

Karatasi ya malipo inaonyesha Lenolkulal 'anajua kupata maslahi binafsi ya moja kwa moja katika kandarasi kati ya Oryx na Samburu kwa usambazaji wa mafuta.

View Comments