Utafanya nini iwapo mpenzi wako wa zamani atakurudia miaka mine baadaye akitaka muendelee na uhusiano kama ilivyokuwa hapo awali tayari yeye akiwa na watoto wawili?
Ndio masaibu ya Denis Kasuvi ambaye aliachwa hoi na Magdaline miaka minne iliyopita baada ya kupoteza kazi yake na sasa amerejea mtaani akidai kwamba bado anampenda na yuataa waendelee na mapenzi yao. Denis haa haamini kwamba Mag ana ujasiri wa kusema kitu kama hicho ikizingatiwa kwamba tayari amekuja na watoto wawili! Itakuaje aanze kubeba mzigo ambao haujui gharama wala uzito wake?
Mwenyewe anasema Mag alikuwa mpenzi wake wa kwanza na ndio uliokuwa uhusiano wake ambao ulidumu muda mrefu na kumuacha na athari kubwa kwani tangia wakati huo mwaka wa 2015 ,hajawahi tena kuamua kujitosa katika uhusiano na mwanamke mwingine . Anasema tangu alipoachana na Mag ,aliamua kujipenda na amekuwa akiendelea na juhudi za kujiboresha ili kuafikia ndoto zake . Magdaline alimuacha wakati alipopoteza kazi yake na wakati huo hali ya maisha ilikuwa ngumu . Hajawahi kuelewa usaliti huo wa kumpenda mtu wakati war aha kisha kumtoroka wakati wa shida .
Licha ya hayo ,Denis anasema imekuwa vigumu kumsahau Mag na sasa hali inazidishwa kuwa tete Zaidi wakati huu amhapo anamuona kila wiki wanapokutana kighafla dukani au kila mtu akienda shughuli zake . Magdaline alienda Dubai pindi walipotengana na haijulikai alirejea linin a ni vipi alivyopata watoto wawili hadi kufikia sasa
Denis ana maswali mengi ya kumuuliza lakini anaogopa kufanya hivyo itakuwa ni kama tena kufungua machungu ya kale . Ingawaje bado anamjali ,amesema itakuwa vigumu kwake kukubalia warudiane kwa sababu mengi yamebadilika na huenda kilichofanyika miaka mine awali kikajirudia .
Hofu yake ni kwamba kuendelea kuishi katika mtaa moja ma Magdaline na kumuona kila wakati ni hatari ambayo huenda akajipata amelegea moyo na kumsamehe kisha ajipate tena naye . Anasema itakuwa sio sawa kurudiana naye kwa urahisi hivyo hasa ikizingatiwa kwamba tayari ni wazi amekuwa na mahusiano na mwanamme ambaye wamezaa naye watoto wawili na itakuwa kama kuingilia uhusiano wa mtu .
Magdaline kwa upande wake hana aibu kwani amezidi kuzungumza na rafiki zao wa pamoja wa zamani ni kana kwamba hakuna kikubwa kilichofanyika huku akiwaambia wanaotaka kusikiza jinsi yungali anavyompenfa Denis . rafiki zao wengi wanashangaa kilichomfanyikia kwani baada ya kumuacha Denis hoi alipopoteza kazi ,Mag amerudi kwa kishindo bila kujali kwamba alivuruga hisia za mwenzake na sasa anamletea tena zigo la kuja na watoto.