Je ni jambo lipi ambalo umewahi fanyiwa na mpezni wako na hutawahi sahau katika maisha yako.
Kuna baadhi ya watu ambao waliachwa na makovu katika mili yao baada ya kupigana na wapenzi wao.
Mwanamume mmoja aliwaacha wanamitandao midomo wazi baada ya kufichua na kusimulia yaliyomkumba baada ya kupigana na mpenzi wake.
"Aliyekuwa mpenzi wangu alinichapa, alikuwa anakuja kila siku akiwa amelewa, nikiwa naye sijawahi jinunulia kiatu hata ya mia mbili nilikuwa nafana kazi ya mjengo, nikitoka naenda kuuza mahindi ili tuweze kupata pesa
Nilikusanya pesa za kuenda kujenga nyumbani, zikafika elfu mia mbili, baada ya mpenzi wangu kuona pesa zimekuwa nyingi, alinichapa mpajka akaning'oa meno
Si hayo tu alikuwa ananipa kichapo cha mbwa kila siku hadi mgongo wangu una alama ambazo nilipokea kutokana na kichapo hicho
Sasa anataka turudiane," Alileza Mwanamume huyo.
Je ni maoni yapi unaweza kumpa mwanamume huyo, je arudiane na mpenzi wake au amuache tu.