In Summary
  • Je sodo zinaweza watia wasichana motisha wa kukaa shuleni?
  • Wanawake na wasichana ambao wanapata changamoto na Usimamizi wa Usafi wa Hedhi pia watapata athari mbaya kwa maeneo mengi ya maisha
high school

Usimamizi Mbaya wa Usafi wa Hedhi ni moja ya maswala muhimu ambayo huishia kuathiri kujithamini kwa msichana na ukosefu wa upatikanaji wa pedi za usafi pia imetajwa na tafiti anuwai kama mmoja wa wachangiaji wa mimba za utotoni haswa katika kaya masikini na vijijini Kenya, wakati wasichana wanapaswa kushiriki katika tabia hatari za ngono kupata au kununua pedi.

Wanawake na wasichana ambao wanapata changamoto na Usimamizi wa Usafi wa Hedhi pia watapata athari mbaya kwa maeneo mengi ya maisha; zinazohusiana na haki za binadamu za wanawake na wasichana, pamoja na haswa haki za afya, kazi na elimu, na pia usawa wa kijinsia.

Kulingana na uchunguzi wangu wasichana wengi hupata mimba huku wakitafuta pesa za kununua sodo kwa maana wazazi wao hawana mapato mema au mapato ambayo yanweza kuwanunulia sodo kila mwezi.

Licha ya wao kutafuta hizo pesa huwa wanajipata katika mtengo wa kuwa na ujauzito.

Mapema mwaka huu waziri wa elimu George Magoha alisema kwamba wasichana wa shule watapewa sodo za bure ili waweze kubakia shuleni na wasiwe na changamoto katika masomo yao.

Lakini swali kuu ni je sodo zitawatia motisha wasichana kusoma na kusalia shuleni bila tashwishwi yeyote?

Wakati wa janga la corona tumewaona asilimia kubwa ya wasichana wakiwa na ujauzito licha ya umri wao mdogo.

Huku ni kizungumza na mmoja wa wasichana ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha tatu alikuwa na haya ya kueleza.

" Karne hii ya sasa ni vigumu sana kumuona msichana wa shule hana sodo, lakini kuna asilimia kubwa ambayo huteseka wakiwa wamenyamaza kama hawana sodo, lakini kama marafiki wazuri baadhi yao huwa tunawasaidia ili waweze kuendelea na na masomo kama sisi

Jambo moja ambalo mwalimu mmoja alitufunza kupata hedhi si ugonjwa bali ni kuonyesha wewe ni mwanamke akamili

Tukieza pewa sodo za bure na wizara ya elimu inaweza kuwa imewasaidia watu wengi na wasichana wengi ambao huteseka kimya kimya," Aliongea Mwanafunzi huyo.

Nilifunga virago vyangu na kuzungumza na mama ambaye ana mwanafunzi katika shule ya upili ya st Augustine Mlolongo, kwa upande wake alikuwa na haya ya kueleza na kusema,

"Kama vile wizara ya afya ilisema kwamba itatoa sodo za bure watakuwa wamefanya mzuri kwa maana wasichana wengi hasa wenye wanaishi katika maisha duni huwa wanakosa shule kwa siku kadhaa ili hedhi yao iishe

Najua kuna watu watasema karne hii ya saa ni vigumu sana wasichana kukosa sodo lakini kwa kweli huwa wanakosa na wanatia bidii kaika masomo yao

Kile naweza ambia wasichana wa shule ni wasome kwa bidii, na waache mambo ya mapenzi na kama umepatwa na hedhi ambaia mzazi wako ukiambiwa mwanamume hatakusaidia bali ata kupa mzigo mwingine ambao utakaa nao milele

Pia na washauri waazi wawalinde wasichana wao na kuwaelimisha kuhusu hedhi,"

 

 

 

View Comments