In Summary
  • Utafiti  awali  na wa mwaka jana ulinaonyesha kwamba unyanyasaji wa nyumbani uliongezeka wakati wa janga la covid 19
  • Njia za kushughulikia na kupambana unyanyasaji wa nyumbani
32268302-stop-domestic-violence-word-cloud-shape-concept

Utafiti  awali  na wa mwaka jana ulinaonyesha kwamba unyanyasaji wa nyumbani uliongezeka wakati wa janga la covid 19.

Hii ililetwa na ukweli kwamba watu waliishi ndani kwa muda mrefu na kukaa pamoja tangu asubuhi hadi usiku wakati wa lockdown.

Katika ulimwengu wa sasa, wanandoa  mara chache hutumia muda wao pamoja kwa sababu kwa kawaida hufanya kazi katika maeneo yao ya kazi.

Wakati ambao huwa pamoja ni wikendi au siku ya sikukuu ya umma, hii ilionyesha kwamba watu wengi hawajazoeana na wake au waume zao huku unyanyasaji na vurugu vikiripotiwa kila siku.

Lakini katika makala haya tutazingatia njia ambazo unaweza shughulikia na kupambana na unyanyasaji wa nyumbani.

1.Omba ushauri

Ukiona mambo katika ndoa yako inakwenda mrama haya basi funga viatu mshipi na kuenda kuamba ushauri kwa mtaalam na wala sio mwenzako kwa maana kuna wale watakupotosha na kuharibu ndoa yako.

2.Jua thamani yako

KUna baadhi ya watu ambao watakaa kwenye ndoa ambayo ananyanyaswa kwani wanaogopa kile marafiki aua jamaa zake watasema.

Lakini kitu cha maana unapaswa kujua ni thamani yako na wala sio kile watu wanasema, kila mtu lazima awe nathamani maishani mwake.

3.Achana na ndoa yako

Anza kufanya mpango wa usalama. Tafuta makao ya ndani na ambayo utapata usalama wako Weka nyaraka muhimu, kitambulisho, na pesa taslimu huko pamoja na nguo.

Ikiwa una watoto, ondoka nao. Kusamehe hitaji la vurugu ndani yako. Kisha usamehe kwa mwenzi wako mkali na uondoke. Hii ndio njia yako ya uponyaji na amani.

4.Kumbuka uponyaji ni mchakato

Endapo utaondoka kwenye ndoa yako usisahau kwmba huwezi sahau yale umetendewa na siku moja, jipe muda wa kupona.

Mara kwa mara wanawake wamekuwa wakipasa sauti endapo wana nyanyaswa na kusahu kwamba pia kuna baadhi ya wanaume ambao wanayanyaswa wakiwa wamenyamaza ili wasipokee kejeli kutoka kwa jamii.

 

 

 

View Comments