Image: AFP

Kuwepo na ongezeko kubwa la sukari katika mpangilio wako wa chakula ni mbaya kwa afya yako, muda mwingine husababisha dalili zisizokuwa rahisi kutafsiriwa.

Matumizi ya sukari kwa mataifa mengi ya Ulaya, yameendelea kuzorota kwa kipindi cha hivi karibuni.

Inaweza kuchochewa na mambo mbalimbali, kupoteza ladha kwenye chakula inayotokana na mfumo wa maisha ambayo mtu ameamua kujiwekea huku ikichangiwa na kiasi kidogo cha wanga.

Uelewa wa ongezeko la matumizi ya sukari nyingi pia unaweza kushuka.

Kupunguza kiwango kikubwa cha utumiaji wa vyakula vyenye sukari unafaida kubwa sana hata katika kupunguza uzito na pia afya ya kinywa.

Ila watu wengi wamekuwa wakiripoti matokeo hasi baada ya kuchukua maamuzi ya kutokula chakula kingi chenye sukari.

Maumivu ya kichwa pamoja na mabadiliko ya hisia huwa yanatokea.

Mabadiliko haya katika mwili huwa ni vigumu kuyaelewa ila wataalamu wanasema kuwa yanaweza kutokana na namna ubongo unavyokuwa umepokea baada ya kupata taarifa ya chakula chenye sukari.

Image: ALAMY

Vyakula vya wanga vipo kwenye mfumo tofauti ikijumuisha na sukari, ambayo hutokea kwenye vyakula tofauti, kwa mfano fructose kwenye matunda na lactose kwenye maziwa. Sukari ipo zaidi kwenye miwa,sharubati na asali zenyewe zina glukosi.

Kutokana na uzalishaji mkubwa wa chakula, sukari imeendelea kuwekwa ili kumvutia mlaji.

Zaidi ya ladha iliyoboreshwa, sukari ina athari kubwa ya kibaolojia katika ubongo. Athari hizi ni muhimu sana hata imesababisha mjadala kuwa pengine inaweza kupelekea uraibu wa sukari ila bado wataalamu wanafanyia uchunguzi.

Sukari inaamsha vipokezi vya ladha tamu mdomoni ambayo mwishowe husababisha kutolewa kwa kemikali ambayo inajulikana kwama 'Dopamine hufanya kazi kwenye neva na kupitisha ujumbe kwenye ubongo.

Vichochezi vinavyoletwa huathiri sehemu kubwa ya ubongo ambapo inamtengenezea mtu furaha ya muda mfupi lakini hugeuka kuwa tabia, hii ina maana kuwa tunaendeshwa na tabia zinazojirudia. Dopamini inatuchochea kula vyakula hata ambavyo sio vizuri kwa afya.

Uchunguzi uliofanyika kwa wanyama pamoja na binadamu unaonyesha namna ambavyo inaathari kubwa, kiwango kikubwa cha utamu kina uwezo wa kuushawishi mwili kuliko hata dawa za kulevya. Sukari ndio yenye uwezo huu haijalishi ni njia ipi imeingia mwilini iwe kwa kula au kuchomwa kwenye miriija inayopitisha damu.

Utafiti umeonyesha panya anapokuwa ametumia kiwango kikubwa cha Sukari inaweza kubadilisha uwezo wa ubongo wake kutokana tu namna 'dopamine' inavyojiendesha.

Image: GETTY IMAGES

Ni dhahiri kuwa sukari ina madhara makubwa sana kwa binadamu, ndio maana sio jambo la kushangaza kwa mtu kupata madhara hata pale anapotumia kiwango kidogo cha sukari.

Mtu kuumwa kichwa, sonona na uchovu yameripotiwa zaidi hii ina maanisha kuwa kuacha kutumia sukari inaweza kufanya ukose nguvu na hata uwezo wa kufikiri kupungua.

Viashiria vya awali bado havijaweza kupatiwa ufumbuzi, lakini bado wanasanyansi wana amini kuwa vina uhusiano na ubongo. Licha ya kwamba 'uraibu wa sukari' ikidaiwa kupunguza vichocheo vyote vya uchovu na kuumwa kichwa.

Tafiti nyingine zilizofanywa kwa wanyama zimeonesha uraibu wa matumizi ya sukari ina uhusiano wa karibu na madawa hatari ya kulevya ila bado haijajulikana kuwa yanaweza kufanana na kwa binadamu.

Sukari inapoondolewa kwenye chakula ,kunakuwa na punguzo kubwa la matatizo yanayosababishwa na kemikali kwenye ubongo.

Unapojiwekea malengo ya kupunguza kiwango cha sukari, ni vyema pia kujua kwamba sukari sio mbaya kwenye mwili wa binadamu na katika safari ya kubadilisha mlo ni vyema pia kuzingatia uwiano wa chakula chenye afya pamoja na kufanya mazoezi.

View Comments