In Summary

• Simu hii ya gharama ya chini sasa iko nchini Kenya, na kupanua uwepo wa simu za chapa ya realme kwenye soko la rununu la Kenya.

realme CY21

Watengenezaji wa simu wameweka mikakati wakizingatia  changamoto za kifedha za wateja, na kutilia maanani uwezo wa kumudu na kuvutia mauzo.

Moja ya kampuni za simu zinazotekeleza mkakati huu ni realMe ambayo imezindua safu ya bidhaa katika orodha hii, na ya hivi punde ni C21Y, simu ya kisasa aina ya smartphone ya kwanza ulimwenguni yenye hakikisho la TÜV Rheinland.

Simu hii ya gharama ya chini sasa iko nchini Kenya, na kupanua uwepo wa simu za chapa ya realme kwenye soko la rununu la Kenya.

Uzinduzi huo unafuatia utendaji mzuri wa realme C11 kutoka kwa kiwango cha kwanza cha C-Series ambayo ilizinduliwa mnamo mwaka 2020 na C11 mwaka 2021 ambayo iliingia mapema mwaka huu.

“Wateja wetu wa Kenya wametufanya tujivunie. Kasi waliyopokea bidhaa zetu inaweka saini wazi juu ya kile tumekuwa tukisema kila wakati kuhusu sisi kuelewa mahitaji yao na kuwa wema kwenye mifuko yao, ”meneja masoko wa realme Kenya Mildred Agoya alisema.

realme C21Y inakuja na mfumo ulioboreshwa zaidi. Ina  betri lenye uwezo wa 5000mAh na kutunza nishati kwa hali ya juu.

Inaboresha hadi kuweka kamera tatu na kamera ya 5MP ya selfie. Pia ina Prosesa ya UNISOC T610 12nm, 6.5 ”HD + Mini-drop Full screen, sensa ya kidole na 2 + 1Slot yote haya yamepangwa maridadi  ndani ya umbo la rangi nyeusi na bluu kwa bei rahisi ya Shilingi 12,399 na Shilingi 13, 700 kulingana na uwezo wa uhifadhi kwenye simu.

“Tunajua wateja wetu wanataka nini. Tunajua pia kwamba mitindo ya teknolojia inaendelea kubadilika. Siku zote tunakimbia kujaribu kufuata mwenendo ili kuhakikisha kuwa wateja wetu wanafurahi, "Agoya alisema.

Kampuni hiyo imepanga kuzindua simu ya toleo la realme GT Master, ambayo ni simu ya kiwango cha juu katika mwezi moja ujao ili kukidhi hitaji lijalo la muundo wa hadhi ya juu.

View Comments