In Summary

•Muogeleaji mmoja ambaye amekuwa akihusika katika kuiopoa miili hiyo amesema kwamba baadhi ya miili ilikuwa imekatwakatwa, imefungwa kwa kutumia Kamba na kutiwa katika ,magunia.

Chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Yala
Image: TWITTER

Wasimamizi wa hospitali katika eneo la magharibi mwa Kenya wamethibitisha kwa BBC kuhusu uwepo wa miili isiyopungua 20 iliooza katika chumba kimoja cha kuhifadhia maiti karibu na mto ambapo miili hiyo inadaiwa kuopolewa katika wiki za hivi karibuni.

Lakini ni nini haswa tunachokijua kuuhusu miili hiyo kufikia sasa?

Shirika la haki za kibinadamamu la Haki Afrika , lilifichua kwamba kwa wiki kadhaa sasa wakaazi wamekuwa wakiopoa miili kutoka mto Yala ambao maji yake yanaelekea katika ziwa Victoria.

Muogeleaji mmoja ambaye amekuwa akihusika katika kuiopoa miili hiyo amesema kwamba baadhi ya miili ilikuwa imekatwakatwa, imefungwa kwa kutumia Kamba na kutiwa katika ,magunia.

Muogeleaji huyo ameaongezea kwamba tangu katikati ya mwaka uliopita amekuwa akiiopoa miili na anaamini kwamba huenda kuna miili zaidi inayooza katika mto huo.

'Maji hayo hutumika kwa matumizi ya binadamu'

Maji ya mto huo yamekuwa yakitumiwa na Wakenya katika eneo hilo kwa matumizi ya nyumbani

Tayari mkuu wa hospitali ya kaunti ya Yala iliopo kilomita 40 kaskazini magharibi mwa mji wa Kisumu , amethibitishia BBC kwamba chumba cha kuhifadhia maiti katika hopsitali hiyo kinamiliki miili 21 ambayo haijapata wenyewe.

Kufikia sasa haijulikani ni nani anayehusika na mauaji hayo ama miili hiyo inatoka wapi .

Hatahivyo maafisa wa polisi nchini Kenya wanasema kwamba kisa hicho kimekuwa kikiendelea kwa mwaka mmoja sasa. Msemaji wa polisi ameambia BBC kwamba uchunguzi bado haujabaini watu hao au lengo la mauaji hayo.

Wameongezea kwamba kufikia sasa hawawezi kubaini ni miili mingapi ilyoopolewa katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita , huku wasimamizi wa hospitali ya Yala wakisema kwamba miili ambayo haina watu huzikwa kila baada ya siku 90.

Tayari baadhi ya Wakenya wanataka majibu huku kukiwa na madai kjutoa kwa wakaazi wa Yala kwamba miili mingi iliyoopolewa ilikuwa na majeraha ya mateso.

Je Mashirika ya haki za kibinadamu yanasemaje?

Kufuatia malalamishi ya Wakenya katika mitandao ya kijamii , shirika la haki za kibinadamu la Haki Afrika lilielekea katika kaunti ya siaya ili kufuatialia tukio hilo.

Linasema kwamba liligundua miili 21 katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya kaunti , ambapo miili mingi ilikuwa imefungwa kamba na mingine kupatikana katika magunia huku mingine ikiwa na alama za kukatwa na mingine ikiwa imefungwa nailoni katika vichwa.

Shirika hilo linasema kwamba lilithibitisha na kituo hicho cha kuhifadhia maiti kwamba mnamo mwezi Oktoba kilizika miili tisa katika kaburi la pamoja.

Katika mto Yala , Haki Afrika imesema kwamba muogeleaji ambaye amekuwa akiopoa miili hiyo amesema kwamba tangu mwezi Julai 2021, aliopoa miili 31 - miili kumi ikiwa ndani ya gunia.

Katika mto huo wanaharakati hao walithibitisha miili miwili iliokuwa ikiolea katika maji ya mto huo ambayo pia hutumika kwa matumizi ya nyumbani na jamii za eneo hilo.

Shirika hilo la haki za kibinadamu hivi sasa limetoa wito wa kutaka kubaini miili hiyop. Vievile limeitaka serikali kufichua ni nani anayehusika na mauaji hayo na kutupwa kwa miili hiyo katika mto huo ili kuchukuliwa hatua kali.

View Comments