In Summary
  • Kitendawili cha miili ya watu iliopatikana katika mto Yala
Mto Yala
Image: MAKTABA

"Nimeona kaka yangu muda mfupi uliopita. Sura zetu zinafanana hata mdomo. Miguu pia nimeiona, huyo ni ya kaka yangu, sina shaka ni yeye."

Irene Waheto aliyefadhaika alisema mara baada ya kutoka katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali huko Yala, magharibi mwa Kenya.

Takriban miili 19 ambayo haijadaiwa imekuwa ikisubiri kutambuliwa. Ziliopolewa Mto Yala katika kipindi cha miaka miwili iliyopita zikiwa katika hatua tofauti za kuoza.

Bi Waheto anapiga simu kwa familia yake huko Nyeri, mji ulio karibu kilomita 300 eneo la kati ya Kenya.

"Ni Ndirangu, Nina uhakika ni yeye ," huku akilia.

Lakini jinsi mwili wake ulivyoishia kupatikana katika mto huo ulio mbali na kwao mpaka sasa haijabainika.

Bi Waheto ananiambia kakake alitoweka Novemba mwaka jana alipokuwa akisafiri kutoka mji mkuu, Nairobi, kwenda Nakuru - lakini hiyo ni takriban kilomita 200 kutoka mahali ambapo mwili wake ulipatikana.

Tangu wakati huo familia yake imekuwa ikipekua vituo vya polisi na vyumba vya kuhifadhia maiti karibu na miji hiyo miwili - lakini si katika sehemu hii ya mbali zaidi ya magharibi mwa Kenya.

Wazo la kuangalia hapa lilikuja wakati, Jumatatu, wanaharakati wawili wa haki za binadamu kusema kwamba miili ambayo ilikuwa imepatikana katika Mto Yala katika miezi ya hivi karibuni ilikuwa bado katika chumba cha kuhifadhia maiti.

Bi Waheto, ambaye alikuwa akiishi karibu na hapo tangu aolewe zaidi ya muongo mmoja uliopita, aliambiwa aende katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Yala ili kuangalia. Lakini ilionekana kutowezekana kwamba kaka yake angekuwa hapa, maili nyingi kutoka mahali alipoonekana mara ya mwisho.

Lakini ukweli wa mambo ni kuwa alipatikana hapo.

Bi Waheto anakaa kwenye nyasi na kuanza kulia, akitoa sauti ambayo hupelekea kila mtu karibu naye kujawa na hisia.

Sio yeye pekee anayemtafuta jamaa aliyepotea na sio yeye pekee anayeshangazwa na jinsi maiti ilivyoishia kwenye Mto Yala.

Ben Chepkwony alisafiri zaidi ya kilomita 100 kumtafuta kakake, Philemon, ambaye anasema alipotea mwezi uliopita kwenye barabara kati ya Nairobi na Nakuru..

Mabaki yake pia yaligunduliwa miongoni mwa miili iliyoopolewa kutoka Mto Yala, na Bw Chepkwony ameshindwa kuhimili majonzi.

"Sijui ni nani anayewaua watu hawa na kuwaacha [hapa]," anasema na kunyamaza kwa muda mrefu na kupumua kwa kina kati ya sentensi.

"Hii si Kenya ya kidemokrasia tunayotamani kuishi. Nimechanganyikiwa sana na nchi hii. Na sitaikubali hata kidogo."

Bw Chepkwony hafafanui anachokataa kukubali - kifo cha kaka yake au kuishi katika nchi ambayo kutoweka na vifo visivyoelezeka imekuwa kawaida. Polisi wanatuhumiwa kuhusika na vifo hivyo na baadhi yao wamekuwa wakianziwa na wanaharakati wa haki juu ya miili iliyopatikana huko Yala.

Boniface Mwangi, mmoja wa wanaharakati wawili waliogundua kuwepo kwa miili hiyo kwa mara ya kwanza, alisema katika mjadala wa Twitter kwamba hakuna Mkenya wa kawaida aliye na uwezo wa kuua mtu na kusafirisha mwili huo umbali wa kilomita 200 kwenda kuutupa mtoni.

'Vifo na kutoweka'

Mwanaharakati mwingine, Khalid Hussein, kutoka shirika linaloitwa Haki Africa, alisema jukumu la kufanya jambo fulani liko kwa polisi: ama wanapaswa kujieleza au kujua ni nani anahusika na mauaji haya.

Nchini Kenya, vikosi vya usalama kwa kawaida huwa miongoni mwa washukiwa wa kwanza wakati vifo vinavyotiliwa shaka na kutoweka vinapotokea - kwa sababu za msingi.

Mashirika ya haki za binadamu yamenakili visa kadhaa vya mauaji yanayohusishwa moja kwa moja na maafisa wa usalama.

Mnamo 2019, Human Rights Watch iliripoti kwamba polisi waliwaua zaidi ya wanaume na wavulana 21 katika maeneo ya watu wa kipato cha chini jijini Nairobi "bila uhalali, wakidai kuwa walikuwa wahalifu".

Missing Voices, kundi la mashirika yanayorekodi mauaji ya nje ya mahakama nchini Kenya, linasema Wakenya 167 waliuawa au kutoweka wakiwa mikononi mwa polisi mwaka wa 2020.

Hali ambayo baadhi ya miili hiyo iliyoopolewa mtoni pia inazua maswali.

Kulingana na mzamiaji aliyewatoa, wengine walikuwa wamewekwa kwenye magunia, ambayo yalikuwa yameshonwa. Wengine walikuwa na mifuko ya plastiki juu ya vichwa vyao - yote ikiwa ni dalili za mateso na mauaji, kulingana na Haki Africa.

"Serikali ina jukumu la kueleza umma kile kinachoendelea," mwanaharakati wa haki za mitaa Fred Ojiro anasema.

"Miili iliyopatikana Yala sio ya wakazi wa hapa, ni ya watu wa mbali sana. Kwa hiyo hivi sio vifo vya kawaida. Ni lazima serikali ijitokeze na ieleze ni kwa nini miili mingi imetanda hapa."

Licha ya mashaka hayo hakuna ushahidi kuwa vikosi vya usalama vilikuwa na uhusiano wowote na miili iliyoipolewa katika Mto Yala. Polisi wanasema baadhi ya watu hao huenda walikufa maji au ni wahasiriwa wa wahalifu na wameanzisha uchunguzi.

 

View Comments