In Summary

• Ndindi ambaye kwa sasa ni mwanzilishi wa shirika la Present Fathherhood amesema kwamba mke wake alikuwa anaandika ratiba ya vitu ambavyo lazima angemfanyia vile alikuwa akitaka.

• Ndindi alisema kwamba jamii imefanya wanaume kuishi na kuvumilia katika mahusiano ya kikatili kuwa jambo la kawaida kwa sababu wanachekwa pindi wanapojaribu kusema kuwa wanadhulumiwa.

Jeff Ndindi
Image: HISANI

Mwanaume mmoja ameelezea vile aliwahi tendewa ukatili katika ndoa na mke wake.

Mwanaume huyo aliyetambulika kwa jina Jeff Ndindi akizungumza katika runinga moja nchini Februari  2, ameelezea kwamba mke wake alikuwa mkatili wa kupindukia na alikuwa anamratibia vitu vya kumfanyia.

Ndindi ambaye kwa sasa ni mwanzilishi wa shirika la Present Fathherhood amesema kwamba mke wake alikuwa anaandika ratiba ya vitu ambavyo lazima angemfanyia vile alikuwa akitaka.

Amezungumza kwa uchungu ni kwa jinsi gani alikuwa anaudhika bila kuonesha kwa sababu mwanamke wake alikuwa anataka amfanyie vitu mpaka vile ambavyo alikuwa anajua kabisa wanawake wana uwezo wa kujifanyia bila kusaidiwa.

Jeff alisema kwamba matakwa mengine kutoka kwa mke wake yalikuwa ni vitu vya kusadikika tu na ameelezea kwamba hata kuzungumzia suala hilo na mpenzi wake ilikuwa ni tatizo kubwa kwa sababu mke huyo angeanza kumuelezea vitu ambavyo wanaume ni sharti wavifanye kwa njia yoyote ile.

Katika mazungumzo hayo, Ndindi alisema kwamba jamii imefanya wanaume kuishi na kuvumilia katika mahusiano ya kikatili kuwa jambo la kawaida kwa sababu wanachekwa pindi wanapojaribu kusema kuwa wanadhulumiwa.

Jeff ameelezea kwamba mwanamke wake alikuwa anataka kufanyiwa vitu vingi tu, mahitaji ambayo yalikuwa yanazidi uwezo wake wa kifedha.

“Kulikuwa na matarajio Zaidi ambayo yalileta shinikizo zisizohitajika. Alikuwa na orodha ndefu ya vitu alivyokuwa akitarajia mimi kuvifanikisha, ikiwemo tabia na mambo mengine, na mara zote katika orodha hiyo, matarajio yote yalikuwa yakianza na ‘mwanaume’… na jamii yetu imerahisisha sana wanaume kuwa kwenye mahusiano yenye ukatili hivyo kama mwanaume, utakuwa unahangaika ili kukudhi matarajio hayo,” alieleza Ndindi.

Mkurugenzi huyo wa Present Fatherhood alisema baada ya kushindwa kustahimili, ilimbidi ajitoe huko kimya kimya kwa ajili ya kujali maslahi ya utulivu wa akili yake.

View Comments