logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kazi ya Mungu haina makosa! Mambo yanayofanywa na wanawake na kuwashangaza wengi

Achana na wale waliopoteza uzuri wao wa asili wakijaribu kufanya upasuaji wa plastiki.

image

Habari03 April 2022 - 10:56

Muhtasari


  • Wanawake wengine hufanya mambo haya ili kujistarehesha wakati kwa wengine, yote ni juu ya nani atafurahi kuwaona

Hakika utashtuka unapoona mambo ambayo wanawake hufanya ili Kuwavutia wanaume.

Wanawake wengine hufanya mambo haya ili kujistarehesha wakati kwa wengine, yote ni juu ya nani atafurahi kuwaona.

Kuna wanawake wameharibu ngozi zao wakijaribu kupaka rangi. Wengine wameishia na migongo isiyo sawa kujaribu kuwafanya wakubwa.

Achana na wale waliopoteza uzuri wao wa asili wakijaribu kufanya upasuaji wa plastiki.

Ni kweli kwamba wanaume wanathamini sifa fulani katika wanawake. Wengine wanathamini sehemu kubwa za nyuma, wengine wanawake wembamba wakati kwa wengine, wanawake wa asili ni wa kutosha kwao.

Je, huoni hii ni nyingi sana? Kwa nini wanawake huchagua kupitia maumivu ili kuushangaza ulimwengu?

Ni mambo gani mengine ya kichaa ambayo Wanawake hufanya ili kuifanya miili yao ionekane wanavyotaka?

Haya hapa baadhi ya mambo ambayo wanawake hufanya na kuwaacha wengi midomo waza;

1.Kubadili rangi ya ngozi

Wanawake wengi wameweza kubadili rangi ta ngozi yao ambapo kwa mimombo inafahamika kama 'bleaching'.

Wengi hufanya haya ili waweze kupendeza mbele ya watu hasa wanaume.

2.Kufanya upasuaji wa plastiki

Sio mmoja au wawili ambao wamefanya upasuaji ili kuurekebisha mwili wao, lakini hawafahamu ya kuwa kazi ya Mungu haina makosa, kwani alikuwa na sababu ya kukuumba jinsi ulivyo.

3.Kuongeza makalio

KUna baadhi ya wanawake ambao hawajabarikiwa na makalio makubwa kwani wao ni wembamba kwa hivyo wanaoneelea ni vyema kuongeza makalio yao ili wapendeze.

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved