In Summary

•Foleni ndefu zimeendelea kushuhudiwa katika maduka ya watoa huduma za simu na maajenti wao kote nchini huku wamiliki wa simu ambao bado hawajasajili laini zao wakijitahidi kutofungiwa nje.

Umati katika duka la Safaricom ukisubiri kuhudumiwa.
Image: SHARON MAOMBO

Wakenya wameendelea kufanya juhudi za dakika za lala salama kusajili laini zao za simu huku muda wa makataa uliotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano nchini (CA) ukiwa umekaribia.

Mamlaka ya mawasiliano ilipeana hadi April 15, 2022 kwa Wakenya ambao hawajasajili laini zao kuhakikisha wamefanya vile.

Foleni ndefu zimeendelea kushuhudiwa katika maduka ya watoa huduma za simu na maajenti wao kote nchini huku wamiliki wa simu ambao bado hawajasajili laini zao wakijitahidi kutofungiwa nje.

CA imefafanua kuwa agizo la kusajili laini za simu litaathiri tu laini ambazo hazijasajiliwa na si watumiaji wote wa huduma mbalimbali za simu kama ilivyodhaniwa hapo awali.

Mkurugenzi Mkuu wa CA, Ezra Chiloba amesema sio sharti kwa Wakenya kutembelea maduka na maajenti wa huduma za simu ili kubaini ikiwa laini zao zimesajiliwa. Amesema watumizi wa huduma za simu wanaweza kutambua ikiwa laini zao zimesajiliwa kwa kupiga *106#

Wale ambao watapata kuwa  laini zao zimesajiliwa wameshauriwa kuendelea na shughuli zao za kawaida.

Watumizi ambao wamekuwa na laini zao kwa zaidi ya miaka 10 wameshauriwa kutembelea watoa huduma wao ili kusasisha data zao.

View Comments