Rais mstaafu Mwai KIbaki
Image: FREDRICK OMONDI

Aliyekuwa rais wa Kenya Mwai Kibaki alifariki siku ya ijumaa akiwa na umri wa miaka 90.

Rais Uhuru Kenyata alitangaza kupitia runinga mbalimbali nchini Kenya.

Lakini mbali na umaarufu wa rais huyu, kuna mambo kadhaa ambayo si wengi wanayafahamu.

Alikua hapendi jina Emilio

Kibaki alizaliwa na Kibaki Githinji na Teresia Wanjiku katika Kijiji cha Thunguri, Othaya, huko Nyeri.

Wamishonari Waitalia walimbatiza jina Emilio, lakini inaonekana hakupendezwa na jina hilo.

Kwa hiyo, alikuwa Mwai Kibaki kwa maisha yake yote. "Emilio" ingejitokeza katika karatasi za kupigia kura, malalamiko ya uchaguzi na hati za kuapishwa.

Alikua kondakta wa basi

Wakati wa kipindi cha likizo alifanya kazi katika kampuni ya magari ya Othaya African Bus Union.

Alikua Mwanafunzi mahiri, alifuzu kwa Shule ya Sekondari ya Mang'u ambapo alikuwa mwanafunzi wa kwanza"A", kati ya 1947 na 1950 alipata ufaulu wa pointi sita katika mitihani yake kidato cha nne.

Alitaka kujiunga na jeshi

Inawezekana kwamba Kibaki angeishia kuwa Jenerali Kibaki lakini mamlaka za kikoloni hazikuwa na nia ya kuwa na wanajeshi kutoka katikati mwa Kenya, nyumbani mwa kundi la Mau-Mau.

Ndoto yake ya taaluma ya kijeshi, iliyochochewa na maveterani waliorejea katika Vita vya Pili vya Dunia, lakini iliyeyuka alipojiunga na Chuo Kikuu cha Makerere, Uganda, ambako alisoma Uchumi, Historia na Sayansi ya Siasa akihitimu mwaka wa 1955 na Shahada ya Kwanza ya Heshima B.A. katika Uchumi.

Siku hizo kulikuwa na kazi nyingi kuliko watafutaji wake. Akiwa na sifa hizo za hali ya juu, alipata kazi katika kampuni kubwa ya mafuta ya Shell kama meneja msaidizi wa mauzo katika Kitengo chake cha Uganda.

Baadaye, alijiunga na Shule ya Uchumi ya London kwa shahada ya Fedha ya Umma na kuhitimu kwa kishindo na kurudi Makerere kama mhadhiri mwaka wa 1958.

RAIS MSTAAFU MWAI KIBAKI
Image: FREDRICK OMONDI

Atajwa na jarida la Times mwaka 1974 kama 'mwenye uwezo wa kuongoza'

1974, alikubaliwa na vita vikubwa vya kugombea kiti cha Donholm kutoka kwa Jael Mbogo ambaye alikua karibu amvue madaraka 1969, na kuhamishia kituo chake cha kisiasa hadi Othaya

Gazeti la TIME lilimtaja kuwa miongoni mwa watu 100 duniani waliokuwa na uwezo wa kuongoza. Na hawakukosea Kibaki angekuwa mbunge wa Othaya hadi 2007 na Rais wa Kenya wa mihula miwili.

Lakini Mwaka 1978 Moi alimtaja kuwa Makamu wa Rais na Waziri wa Mambo ya Ndani.

Alikua anapenda mchezo wa gofu

Kibaki alipenda sana kucheza mchezo wa gofu na alikua mlezi wa klabu ya gofu ya Kenya kwa zaidi ya miaka 30. Aliamini kwamba kwa kutumia mchezo wa dou, ajira nyingi zinaweza kupatikana kwa Wakenya.

View Comments