logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Siri ya Kuishi Muda Mrefu: Pata mke wa pili- Utafiti

Utafiti unapendekeza kuwa siri ya kuishi maisha marefu kunahusishwa na kuwa mke wa pili au zaidi.

image
na Radio Jambo

Makala03 June 2022 - 18:30

Muhtasari


•Utafiti kutoka chuo kikuu cha Sheffield nchini Uingereza unapendekeza kuwa siri ya kuishi maisha marefu kunahusishwa na kuwa mke wa pili au zaidi.

•Kutunza wajukuu, inaonekana, kunawapa wanawake sababu ya kuishi muda mrefu baada ya kushindwa tena kuzaliana.

Utafiti kutoka chuo kikuu cha Sheffield nchini Uingereza unapendekeza kuwa siri ya kuishi maisha marefu kunahusishwa na kuwa mke wa pili au zaidi.

Watafiti kutoka chuo hicho waliwachunguza wanaume wenye umri zaidi ya miaka 60 kutoka nchi 140 zinazotumia ndoa za mitala na wakagundua kwamba waliishi wastani wa asilimia 12 zaidi ya wanaume kutoka mataifa 49 yenye mke mmoja, kwa mujibu wa ripoti kutoka gazeti la Times of India.

Matokeo ya utafiti yaliwasilishwa wiki iliyopita katika mkutano wa kila mwaka wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ekolojia huko Ithaca, New York,

Watafiti waliangalia utafiti wa awali juu ya wanawake kujibu kwa nini wanaume wenye mitala huishi kwa muda mrefu.

Pia Wanasayansi wanaamini kuwa wanawake ambao wamekoma hedhi wanaishi kwa muda mrefu zaidi kuliko mamalia wengine kwa sababu kadiri wanavyoishi ndivyo wajukuu wengi zaidi wanavyolazimika kuwajali.

Kutunza wajukuu, inaonekana, kunawapa wanawake sababu ya kuishi muda mrefu baada ya kushindwa tena kuzaliana.

Kupenda wajukuu, hata hivyo, hakuna faida sawa za kuongeza maisha kwa wanaume kwani wanaume wanaweza kuzaliana katika miaka ya 60, 70 na 80. Hivyo watafiti wanasema, kwamba wanaume wenye wake wengi hupata aina fulani ya athari za baba, wakimaanisha, kadiri wanavyokuwa na wake wengi, ndivyo wanavyozaa watoto zaidi.

Kuzaa watoto huwapa sababu ya kuendelea kuishi muda mrefu zaidi kuliko wanaume wenye mke mmoja ambao mara nyingi huacha kuzaa watoto katika umri wa mapema zaidi, watafiti walihitimisha.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved