Maafisa wa afya wakipima virusi vya corona
Image: PA MEDIA

Sayansi mara nyingi hutubabaisha, wakati mwingine kwa sababu ambazo ni zaidi ya kile kilicho wazi.

Fikiria, kwa mfano, ya kauli hiyo kwamba ukimweka chura kwenye maji ya moto, mara moja utaruka nje, lakini ukimweka kwenye maji ya uvuguvugu na hatua kwa hatua utaongeza joto, hautajua hatari na utapika hadi afe.

Ni sawa na kitu chenye nguvu kiasi kwamba wanasiasa na waalimu maarufu mara nyingi hutumia wito huo kutaka hatua zichukuliwe. Na bila ya shaka sisi tunayastaajabia hayo. Ni mwanasayansi gani alikuja na wazo la kutupa vyura kwenye maji ya moto?

Inaonekana hakuna.

Ingawa inaonekana kama matokeo ya majaribio, kamwe haikuwa hivyo. (Ukweli ni kwamba, kwa mujibu wa wataalamu, mara tu joto lilipomkosesha raha, chura aliyekuwa kwenye maji ya moto angeruka, wakati mwingine asingeweza, kwa sababu, kama kiumbe yeyote aliyeanguka kwenye maji ya moto, angekufa).

Lakini kulingana utafiti mwingine ambao pia unazua utata, panya walikuwa wamewekwa katika mitungi ya maji na kuangalia tu wakati wanazama, hali ni tofauti.

Hii ilifanywa, na mwanabiolojia maarufu, mtaalamu wa saikolojia na mtaalamu wa jeni Curt Richter.

Na kwa wale wetu ambao wamesikia kuhusu majaribio, mara moja walistaajabu "kwa nini alifanya hivyo" bila kuwa na uwezo wa kufuatilia kwa makini matokeo, katika makala yake yaliyochapishwa katika jarida la Psychosomatic Medicine mwaka 1957 kwa kuanza kukabiliana na wasiwasi huo:

"Tulikuwa tunajifunza tofauti katika muitikio wa panya wa kufugwa na wa nyumbani wakiwa na msongo wa mawazo".

Kifo cha ghafla

Richter alichapisha makala yake kwa sababu aligundua panya akiwa kwenye mazingira sawa na utafiti wa Walter Cannon, mmoja wa wataalamu mashuhuri wa sayansi wa karne ya 20.

Katika makala yenye kichwa cha habari "Kifo cha Voodoo", iliyochapishwa mwaka 1942, Cannon alikuwa ametaja matukio kadhaa ya vifo vya ajabu, ghafla na dhahiri vya kisaikolojia, katika sehemu mbalimbali za dunia, ambavyo vilitokea ndani ya masaa 24 baada ya mtu mmoja kukiuka baadhi ya sheria za kijamii au kidini.

"Mbrazili Mhindi aliyehukumiwa na kuhukumiwa na mtu aliyedaiwa kuwa mchawi, asiye na hatia dhidi ya hisia zake kwa tamko hili, alifariki ndani ya masaa kadhaa (...) Mtu mmoja wa asili huko New Zealand ambaye alikula tunda na baadaye akagundua kuwa lilitoka sehemu ambayo ni mwiko. Adhuhuri ya siku iliyofuatilia, alifariki dunia."

Baada ya kupitia kwa makini ushahidi, Cannon alikuwa na yakini na ukweli wa jambo hili na aliuliza mwenyewe: "Inawezekanaje hali ya hofu kuendelea kumaliza maisha ya binadamu?".

Kama Richter alivyoeleza, Cannon alihitimisha kwamba kifo kilitokea kama matokeo ya hali ya mshtuko iliyosababishwa na kutolewa kwa adrenalini kila wakati.

Na alisisitiza kwamba, kama ni hivyo, ingetarajiwa kwamba katika mazingira hayo watu binafsi wangekuwa na, miongoni mwa mambo mengine, kupumua kwao na moyo wao ingekuwa ikipiga kwa kasi sana, "ambayo hatua kwa hatua imesababisha hali ya kujikunja, na hatimaye, mfano, ni kifo kanatokea papo hapo".

Lakini ilibadilika na kwamba utafiti wa Richter na panya ulionyesha kinyume tu.

Kuogelea au kuzama

Katika maabara yake katika Chuo Kikuu cha John Hopkins huko Baltimore, Marekani, Richter alikuwa ameweka panya - wale waliozaliwa, kukua na kufa katika maabara - katika bilauri ambayo hawawezi kutoroka, kuona ni muda gani waliweza kunusurika wakiwa wanaogolea katika maji ya nyuzi joto mbali mbali kabla ya kuzama.

Lakini kulikuwa na tatizo: "Wakati wa nyuzi joto tofauti tofauti, idadi ndogo ya panya waliokufa kati ya dakika 5-10 baada ya kuzama, wakati katika baadhi ya matukio ambako hakukuwa na wa afya, waiogelea kwa hadi saa 81".

Tofauti zilikuwa kubwa sana kwa matokeo kuwa muhimu.

"Suluhisho lilitoka kwenye chanzo kisichotarajiwa: Uvumbuzi wa jambo la kifo cha ghafla ".

Je, inawezekana kwamba Cannon alifanya utafiti miaka kadhaa kabla ya kile kilikuwa kinatokea?

Panya waliokata tamaa

Richter alibadilisha majaribio. Si tu kwamba alianza kupunguza masharubu ya panya, "Kuharibukwa njia yoyote, njia muhimu zaidi ya kuwasiliana na ulimwengu wa nje", lakini yeye alianzisha, mbali na panya kufugwa, aina nyingine na wengine ambao wanapatikana mitaani.

Wakati idadi kubwa ya panya wanaofugwa waliogelea kwa muda wa saa 40 hadi 60 kabla ya kufa, viini (vya aina yote ya panya) "vilikufa kwa muda mfupi sana".

Lakini jambo la kushangaza zaidi ni kwamba wale wa porini, ambao kwa kawaida ni waogeleaji hodari na wazuri, walizama "dakika 1-15 baada ya kuzama kwenye mitungi".

Sasa, unakumbuka kwamba vifo vya ghafla vilitakiwa kutokea baada ya kiasi kikubwa cha adrenalini kilichotolewa kutokana na mfadhaiko kuongeza mapigo ya moyo na kupumua?

Kama ilivyo ada, data zilizokusanywa zilionyesha kwamba "wanyama walikufa na kupungua kwa kiwango cha moyo badala ya kuongeza kasi". Upumuaji ulikuwa wa kasi a chini na joto la mwili lilishuka hadi moyo ukaacha kupiga.

Lakini thamani kama kwamba uchunguzi ulivyokuwa, haikuwa kwa sababu yake kwamba majaribio hayo yalikuwa maarufu.

Panya wasio na matumaini

Kulikuwa na kitu kingine ambacho hakikuweza kupuuzwa.

"Ni nini kinachoua panya hawa?" Alijiuliza. "Kwa nini panya wote wa mwituni wanakufa haraka, wakati wachache tu ya panya kama hao wa nyumbani walikufa?"

Kwanza, alisisitiza, baadhi ya wa mwituni waliokufa hata kabla ya wao kuweka katika maji, wakati watafiti walikuwa nao katika mikono yao.

Ripota huyo alibaini mambo mawili muhimu kuhusiana na jambo hili:

Badala ya kuchochea mapambano, kile Richter alichokiona kuwa kukosa matumaini.

"Ikiwa watashikwa mkononi au watafungiwa kwenye bakuli la kuogelea, panya wako katika hali ambayo hawana ulinzi. Mwitikio huu wa kukosa matumaini unaonyeshwa na baadhi ya panya wakali muda mfupi baada ya kushikwa mkononi "na kuzuiwa kusonga; Wanaonekana 'kukata' tamaa kabisa".

Kwa upande mwingine, kama hisia ya kuishi ingalichochewa katika matukio yote, kwa nini panya wa kufugwa wanaonekana kuwa na uhakika kwamba kama wangeendelea kuogelea wanaweza kujiokoa hatimaye?

Na kwa hawa wote, je panya wanaweza kuwa na "ushindi" tofauti... na hata matumaini?

Pumzi

Richter alibadilisha jaribio hilo tena: Alichukua panya kama hao na kuwaweka kwenye mtungi. Lakini, kabla ya kufa, aliwachukua na kuwatoa nje, kuwashikilia kwa muda, na kuwaachilia kwenda kwa dakika kidogo, na kisha kuwarejesha tena katika maji.

"Hivyo", aliandika, "panya mara moja alijifunza haraka kwamba hali si ya kukosa matumaini; Kisha baada ya hapo wakawa na matumaini tena, na kujaribu kutoroka, wala hawakuonyesha ishara ya kukata tamaa.

Mabadiliko hayo kidogo tu yalileta tofauti kubwa.

Panya walioweza kupata kunusurika kidogo walionyesha kutaka kuogelea zaidi wakijua kwamba hawakuwa wameangamia, kwamba kuna kile kingeweza kuwaokoa, ma wakapigania kuishi.

"Baada ya kuondoa hali ya kukosa matumaini", mtaalamu huyo aliandika, "panya hawafi".

Kifo kwa kuhukumiwa

Lengo la pili la Richter lilikuwa ni kuchangia uchunguzi wa kile kinachoitwa kifo cha voodoo, ambacho, alisisitiza, hakikutokea katika "tamaduni za kizamani", kama Cannon alivyobainisha.

"Idadi kubwa ya vifo isiyoelezeka iliripotiwa miongoni mwa wanajeshi katika majeshi ya nchi hii (Marekani) wakati wa vita. Watu hawa walifariki wakiwa na afya njema. Hakuna patholojia ingeweza kufanywa wakati wa uchunguzi.

"Hapa pia ni jambo la kufurahisha kwamba, kwa mujibu wa Dkt. R. S. Faker, Mganga Mkuu wa Jiji la Baltimore, idadi ya watu wanafariki kila mwaka baada ya kuchukua dozi ndogo ya sumu ya lethal, au baada ya kupata majeraha madogo, na kufariki kama matokeo ya hukumu katika kifo chake".

Majaribio yake yalirudiwa mara kwa mara katika maabara za madawa ili kuchunguza dawa za kitulizo au za kuondoa mshuko-moyo baada ya mtafiti Roger Porsolt kugundua mwaka wa 2005 kuwa panya ambao walikuwa hutolewa walipigana kwa muda mrefu.

Juu ya hayo, Asante kwa mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Kutetea Haki za Binadamu utaratibu wa majaribio ya panya kuogeleakatika mabara kumepungua. Tukio hilo lilikuwa linasumbua kisaikolojia.

Pia, kama majaribio ya chura, ikawa maarufu nje ya mazingira yake ya asili, pamoja na wazo kwamba matumaini huwapa viumbe nguvu ya kupigania maisha yao katikati ya hali ya kukata tamaa.

View Comments