In Summary

• Shinikizo walo nayo wazazi ya kusaka pesa huku wanafunzi wakitarajiwa kuripoti shuleni Alhamisi kuambatana na agizo kutoka kwa waziri wa elimu

Wahudmu wa boda wakisubiri petroli baada ya bidhaa hiyo kupotea mapema mwaka huu
Image: DANIEL OGENDO

Baada ya kura kuu za uchaguzi, sasa wakenya wanajishughulisha kutafuta karo na riziki ili kumudu mahitaji yao hali ambayo imewaweka wengi katika pandashuka.

Shinikizo walo nayo wazazi ya kusaka pesa huku wanafunzi wakitarajiwa kuripoti shuleni Alhamisi kuambatana na agizo kutoka kwa waziri wa elimu Prof George Magoha, limewakosesha usingizi akina pangu pakavu.

Kwa asilimia kubwa ambayo hawana kazi au kipato chao ni kidogo kuwawezesha kukidhi mahitaji yao, inakuwa balaa hasa inapochangia katika ongezeko la maradhi kama vile mzo wa mawazo huku wasijue la kufanya.

Shule zilifungwa kwa kipindi cha wiki mbili ili kuruhusu uchaguzi mkuu  kufanyika. Ni wazi kwamba ghafla hizi kutoka kwa wizara ya elimu zinasambaratisha kiwango cha elimu, wanafunzi hawapati fursa ya kutosha kuudhuria vipindi vya masomo na kutangamana na walimu wao.

Katika kipndi cha masomo 2021/2022 ripoti kutoka kwa wizara ya elimu, inaonyesha kwamba zaidi ya asimia 40 hawakuudhuria masomo kutokana na ukosefu wa karo na hali ngumu ya maisha.

Ilibidi wizara kutengeneza jedwali finyu inatakayojumuisha miula zaidi ya tatu iliw wanafunzi wapate fursa kusoma hasa baada ya mashule kufungua kutokana na virusi vya Corona.

Wengi hutegemea mgao wa CDF ili kufadhili masomo ya watoto wao. Kuna shaka kwamba huenda idadi ya watakao katiza masomo kuongezeka maana serikali mpya itachukua muda kabla ya shughuli kuendelea kawaida.

View Comments