In Summary

•Ukataji wa miti umekuwa chanzo kikubwa cha kupanda kwa kiwango cha joto.

•Wataalamu wa wanamazingira wanaonya kwamba kasi ambayo Wakenya wanakata miti inaangamiza misitu

 


Lori la kubeba miti
Image: Facebook

Ukataji wa miti kihorera ni swala ambalo zimeongezeka sana licha ya serikali kujifunga kibwebwe kukabiliana na uhaini huu.

Iwapo hakutakuwa na marufuku ya ukataji miti haitaji basi taifa litakuwa Jangwa, mifugo itafa, vyakula shambani vitakosa mvua tosha hivyo baa la njaa litashuhudia nchini.

Hofu iliyoko ni jinsi ukataji wa miti umekuwa chanzo kikubwa cha kupanda kwa kiwango cha joto, swala ambalo jopo la wanamazingira linakashifu iwapo miti itaangushwa bila mingine mipya kupandwa.

Wataalamu wa wanamazingira wanaonya kwamba kasi ambayo Wakenya wanakata miti inaangamiza misitu, kukausha vyanzo vya maji na kuathiri hali ya hewa.

Wasiwasi  wanamazingira ni kuwa ukataji miti unaendelea bila mipya kupandwa jambo ambalo ni hatari kwa mazingira katika nchi ambayo idadi ya watu inaendelea kuongezeka.

Kufuatia juhudi za serikali la kuhifadhi mazingira, bado azimio hili litabaki kuwa ndoto tu,iwapo kutakuwa sera madhubuti za kuisimamia misiti.

Lakini wakenya wengi hujihusisha na Uchomaji wa makaa na kupasua mbao kwa minajiri ya kupata riziki, hivyo Serikali zinazopiga marufuku ukataji miti zinapaswa kuwapa wakazi njia mbadala za kupata riziki.

View Comments