logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Jiji la Nairobi lashika nafasi ya 94 katika orodha ya majiji 100 mazuri kote duniani

Afrika Kusini inajivunia majiji mawili kwenye orodha hiyo.

image
na Radio Jambo

Makala25 May 2023 - 05:09

Muhtasari


• Kulingana na utafiti ambao ulifanywa na Brand Finance, Jiji la London Uingereza ndilo la kwanza kote duniani.

• Jiji la Afrika Kusini, Cape Town imeorodheshwa kama chapa bora zaidi barani Afrika

Jiji kuu la Nairobi ,Kenya.

Jiji la Nairobi ambalo ni makao makuu ya taifa la Kenya na kitovu cha kibiashara katika ukanda wa Afrika Mashariki limeibuka katika nafasi ya 94 katika orodha ya majiji 100 kote duniani ambayo yamepigiwa upato kuwa bora Zaidi katika kutangaza na kufanya biashara yako.

Kulingana na utafiti ambao ulifanywa na Brand Finance, Jiji la London Uingereza ndilo la kwanza kote duniani kwa uzuri na utulivu kibiashara, likiwa limejizolea asilimia 84.7 juu ya mia katika kura za maoni ambazo Brand Finance walifanya wakiwashirikisha watu 15,000 kote duniani.

Jiji la Marekani, New York na jiji la Ufaransa Paris yako nyuma sana katika nafasi ya 2 na 3 kati ya majiji 100 katika orodha hiyo.

Jiji la Afrika Kusini, Cape Town imeorodheshwa kama chapa bora zaidi barani Afrika, likiwa limeshikilia nafasi ya 60 kote duniani huku Cairo, jiji la Misri likiwa la pili kwa Afrika na la 67 kote duniani.

Jiji la Johannesburg ambalo pia ni la Afrika Kusini ni la tatu kwa Afrika na la 72 duniani huku Casablanca kutoka Morocco likiibuka jiji la nne na la 76 duniani.

Nigeria na Nairobi wanafunga orodha hiyo ya majiji 100 bora kwa kushika nafasi za 90 na 94 mtawalia.

Nafasi ya Cape Town kama kiongozi wa bara inaweza kuhusishwa na hadhi yake kama jiji la Afrika Kusini linalotembelewa zaidi, likiwa na sifa ya juu na kuzingatiwa kama mahali pa kutembelea.

Uzuri wa asili wa jiji hilo, pamoja na ufuo wake wa kuvutia, milima, na mandhari mbalimbali, huifanya kuwa mojawapo ya maeneo ya kuvutia zaidi ya watalii duniani.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved