In Summary

•Mizoga ya Wanyama wa pori waliosalimu amri  kwa ajili ya hali ngumu ni dhihirisho la maafa ambayo yametokana na kiangazi hiki.

•Wenyeji wanasema wameunganishwa kihisia na wanyama hawa hasa ndovu na kushuhudia vifo vyao ni uchungu usiyoelezeka

Image: BBC

Hali  ni mbaya   katika hifadhi ya kitaifa ya wanyama pori ya Amboseli Kusini mwa Kenya ,ambapo athari za kiangazi ni wazi huku Wanyama wakipata tabu kupata lishe-ardhi ni kavu  na jua halina huruma katika eneo hili.

Mizoga ya Wanyama wa pori waliosalimu amri  kwa ajili ya hali ngumu ni dhihirisho la maafa ambayo yametokana na kiangazi hiki.

Vifo hivyo vimewatamausha wengi na uvundo wa mizoga hiyo ni kumbusho la kila mara la mauti ambayo sasa yamegeuka kuwa jambo la kawaida .

Wanahabari wa BBC walishuhudia tukio la kukatisha tamaa la tembo mkubwa anayedhaniwa kuwa zaidi ya miaka 40 akifa mbele ya macho yao.

Kulingana na wakaazi hili ni jambo la kila siku na linaathiri sio wanyama tu bali pia wanadamu wanaoishi karibu na mbuga hiyo.

Wenyeji wanasema wameunganishwa kihisia na wanyama hawa hasa ndovu na kushuhudia vifo vyao ni uchungu usiyoelezeka

“Tunasikia vibaya, unajua kuna msemo wa Lugha ya Kimasai unasema tunapoona wanyama wakubwa mfano tembo wanakufa basi mambo ni balaa na hatari. " anasema mmoja wa walinzi wa jamii katika hifadhi ya Taifa ya Amboseli.

Ni vigumu sana mtu kuendesha gari hata kwa kilomita moja bila kushuhudia mzoga hapa na pale ndani ya hifadhi hiyo na unaweza kuona mizoga ya Wanyama mbali mbali waliofariki.. 

Licha ya wanyama hao kufa watalii wangali wanaingia kwa wingi kwenye mbuga hiyo na hakuna kinachoonekana kuwazuia kuendesha magari karibu  ili kuona wanyama wa pori wanaowapenda, kwa kuwa wanyama wengi zaidi wanaonekana katika mazingira yao ya asili.

Maafa Amboseli:Mizoga na uvundo wa Wanyama wa pori vyaelezea athari kali za kiangazi
Image: BBC
Maafa Amboseli:Mizoga na uvundo wa Wanyama wa pori vyaelezea athari kali za kiangazi
Image: BBC

Hata hivyo wale wanaokufa wanaendelea kuunda sehemu za takwimu za wanyama ambao wamekufa  kutokana na ukame unaoendelea ambao umekumba sehemu za Kenya.

Tunaelezwa kwamba hali ni mbaya zaidi mwaka huu kwa mara ya kwanza kwa miongo minne .

Wizara ya Utalii na Wanyamapori ya Kenya hapo awali ilisema kuwa nchi hiyo imepoteza tembo 205 mwaka huu pekee kutokana na athari za ukame mbaya unaoshuhudiwa katika nchi hiyo ya Afrika mashariki .

Waziri Penina Malonza anasema maelfu ya wanyama pori, wengi wao wakiwa wala mimea, wamekufa katika mbuga, na hifadhi za nchi kutokana na ukosefu wa maji na malisho.

Anasema hawa ni pamoja na zaidi ya nyumbu mia tano, karibu pundamilia mia nne na nyati hamsini na pia twiga 

Vifo vingi vilirekodiwa Amboseli, Tsavo na katika eneo la Laikipia na Samburu.

Wizara sasa inaomba usaidizi kwa utoaji wa maji na nyasi pamoja na chumvi ili kusaidia wanyama kuishi katika maeneo yaliyoathiriwa zaidi na ukame.

View Comments