In Summary

•Wajackoyah na Mmarekani huyo mwenye asili ya Afrika wamekuwa pamoja kwa takriban miongo mitatu.

•Wajackoyah aliwa kufichua kuwa  mkewe na watoto wake watatu wanaishi nje ya mipaka ya Kenya.

Mke wa Wajackoyah Meller Lee Cheatham katika CUEA mnamo Julai 26, 2022.
Image: EZEKIEL AMINGA

Jumanne jioni mgombea urais wa Roots Party George Wajackoyah alifika katika Chuo Kikuu cha Katoliki cha Afrika Mashariki (CUEA)  ambako mdahalo wa urais unaendelea akiwa ameandamana na mkewe Meller Lee Cheatham miongoni mwa wengine.

Hii ni mara ya kwanza kwa Bi Meller kujitokeza hadharani tangu mumewe alipoidhinishwa kuwania urais mapema mwaka huu.

Wajackoyah na Mmarekani huyo mwenye asili ya Afrika wamekuwa pamoja kwa takriban miongo mitatu.

Mkewe George Wajackoyah Meller katika CUEA mnamo Julai 26, 2022
Image: EZEKIEL AMINGA

Katika mahojiano ya awali, mgombea urais huyo alifichua kuwa mkewe na watoto wake watatu wanaishi nje ya Kenya.

"Nina watoto na mke mzaliwa wa Marekani. Anaishi Marekani na watoto wetu ambao ni watu wazima wanaishi Uingereza," Wajackoyah alisema katika mahojiano na Citizen TV.

Wakati huo alifichua kuwa tayari kuna mpango familia yake kuhamia humu nchini baada ya kupata uraia wa Kenya.

Mtoto wa kwanza wa Wajackoyah anaitwa Ty Luchiri, wa pili anaitwa  Marjorie Luchiri na mzaliwa wa mwisho anaitwa Marz Luchiri.

Mkewe Wajackoyah, Meller katika CUEA mnamo Julai 26, 2022
Image: EZEKIEL AMINGA

Hata hivyo haijathibitishwa ikiwa watoto wa kiongozi huyo wa Roots Party wamo nchini huku uchaguzi mkuu ukiwa umebakisha wiki mbili tu kufika.

View Comments