In Summary

•Watu 1,259 zaidi wamepatikana na virusi vya Corona nchini kutoka kwa sampuli ya watu 8,081 walioweza kupimwa ndani ya kipindi cha masaa 24 yaliyopita.

•Kufikia sasa  watu 1,062,413 wameweza kupokea angalau dozi moja ya chanjo dhidi ya COVID-19 huku 661,314 kati yao wakiwa wamepokea dozi zote mbili.

Waziri Mutahi Kagwe
Image: MOH

Watu 1,259 zaidi wamepatikana na virusi vya Corona nchini kutoka kwa sampuli ya watu 8,081 walioweza kupimwa ndani ya kipindi cha masaa 24 yaliyopita.

Asilimia ya maambukizi nchini kwa sasa ni 15.4% huku jumla ya kesi zilizowahi kuripotiwa ikifikia 203,213. Vipimo 2,132, 355 vimefanyiwa kufikia sasa.

35 kati ya waliopatikana na virusi hivyo ni raia wa nchi za kigeni huku wengine wote 1224 wakiwa Wakenya.

Kaunti ya Nairobi imeendelea kuongoza kwa maambukizi leo hii ikiripoti visa 417. Nyeri inafuata ikiandikisha visa 417, Kiambu 120, Mombasa 96, Nakuru 66 na Kilifi 60. 

Kaunti zingine zimeandikisha visa chini ya 50 kila mmoja.

Wagonjwa 498 wameweza kupata afueni, 357 wakiponea manyumbani huku wengine 141 wakipona kutoka vituo mbalimbali za afya nchini. Kufikia sasa watu 188,936 wamewahi kupona maradhi hayo nchini.

Hata hivyo, Kenya imeandikisha vifo 5 vipya kutokana na ugonjwa wa COVID 19.

Kwa sasa wagonjwa 1,469 wamelazwa hospitalini huku wengine 3,965 wakiendelea kuhudumiwa manyumbani. Wagonjwa 185 wamelazwa katika wadi za wagonjwa mahututi.

Chanjo ya Corona

Kufikia sasa  watu 1,062,413 wameweza kupokea angalau dozi moja ya chanjo dhidi ya COVID-19 huku 661,314 kati yao wakiwa wamepokea dozi zote mbili.

View Comments