In Summary

•Asilimia ya maambukizi nchini kwa sasa ni 9% huku jumla ya visa vilivyowahi kuripotiwa nchini sasa ikifikia 203, 680.

•Wagonjwa 195 wameripotiwa kupata nafuu ndani ya kipindi cha masaa 24 yaliyopita. 

Waziri Mutahi Kagwe
Image: MOH

Wizara ya afya imetangaza kuwa watu 467 wamepimwa na kupatikana na virusi vya Corona kutoka kwa sampuli ya watu 5,217 waliopimwa ndani ya kipindi cha masaa 24 yaliyopita.

Asilimia ya maambukizi nchini kwa sasa ni 9% huku jumla ya visa vilivyowahi kuripotiwa nchini sasa ikifikia 203, 680.

Kenya imeweza kufanya vipimo 2,137,572 kufikia sasa.

Nairobi inaendelea kuongoza kwa maambukizi huku visa 216 vikiripotiwa humo hivi leo. Kaunti za Kiambu na Murang'a zinafuatia na wagonjwa 49 na 43 mtawalia.

Wagonjwa 195 wameripotiwa kupata nafuu ndani ya kipindi cha masaa 24 yaliyopita. 125 kati yao waliponea manyumbani huku wengine 70 wakipinea hospitalini.

Kwa upande mwingine vifo 15 vimeripotiwa kutoka kwa rekodi za vituo mbalimbali vya afya nchini.

Kufikia sasa Kenya imerekodi vifo 3946 tangu virusi hivyo kuingia nchini.

Wagonjwa 3987 wanaendelea kupokea matibabu nyumbani huku wengine 1475 wakiwa wamelazwa hospitalini. Wagonjwa 186 wamelazwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi.

Chanjo

Kufikia sasa watu 1,064,104 wameweza kupata angalau dozi moja ya chanjo dhidi ya Corona huku 662,089 kati yao wakiwa wamepomea dozi zote mbili.

View Comments