In Summary

•Koome amesema idara hiyo inajitayarisha vilivyo kuzishughulikia kesi zitakazotokana na uchagui mkuu wa mwaka ujao nchini Kenya .

•Amekiri kwamba ufisadi miongoni mwa maafisa wa idara hiyo na mrundiko wa kesi bado ni changamoto zinazofaa kushughulikiwa .

Jaji wa mahakama ya rufaa Martha Koome alipofika mbele ya JSC kuhojiwa kuhusu wadhifa wa jaji mkuu, 14/04/2021.
Image: CHARLENE MALWA

Jaji Mkuu wa Kenya Martha Koome amesema idara ya mahakama nchini humo iko huru na itatekeleza kazi yake bila muingilio wowote wa kisiasa .

Katika mahoojiano na BBC Koome ambaye ni mwanamke wa kwanza nchini humo kushikilia wadhifa huo amesema idara hiyo inajitayarisha vilivyo kuzishughulikia kesi zitakazotokana na uchagui mkuu wa mwaka ujao nchini Kenya .

‘Tuko mbioni kujitayarisha kwa mafunzo kuhusu masharti,kanuni na utaratibu wa uchaguzi na sheria zinazofaa kutumika.Tunawahakikishia wakenya kwamba tuko huru hatuna mgombeaji ama wagombeaji tunaowapendelea ‘ amesema Koome .

Koome amesema ana matumaini makubwa ya kufanikisha wajibu wa idara ya mahakama licha ya kuwepo changamoto mbali mbali anapotimiza siku 100 tangu ateuliwe katika nafasi hiyo

Amekiri kwamba ufisadi miongoni mwa maafisa wa idara hiyo na mrundiko wa kesi bado ni changamoto zinazofaa kushughulikiwa .

‘ Nina matumaini tunaweza kufanya vizuri katika idara ya mahakama ,ili kutekeleza jukumu kubwa kama walinzi wa kikatiba,sheria na wateteziwa haki za binadamu’ amesemaKoome

Jaji Koome amesema uhusiano kati ya serikali na idara ya mahakama ni jambo muhimu kufanikisha shughuli za serikali kwa wananchi .

Amesema idara zote za serikali zinategemeana na pana haja ya kulinda uhusiano mzuri.

Koome pia amesema idara ya mahakama nchini Kenya ingali inahitaji majaji Zaidi. Amesema wanahitaji majaji 20 wa mahakama kuu ili kuweza kushughulikia mrundiko wa kesi .

Demokrasia Afrika

Akizungumza kuhusu hali ya demokrasi katika bara la Afrika Koome amesema kuna baadhi ya mambo kama vile mapinduzi yanayofanywa na majeshi kama kikwazo kwa demokrasia .

Hata hivyo amesema Afrika ina sababu ya kufurahia hatua nzuri kama makabidhiano nay a madaraka kwa njia ya Amani katika baadhi ya nchi .

Mtu wa wadhifamkubwa kama yeye hufanya nini wakati hayupo kazini? Koome amesema wakati yuko nyumbani basi;

‘Mimi ni mama nyumbani ,napika ,nawakaribisha wageni wangu,naenda mashambani naenda kanisani na hata kuwafunza watoto jumapili’ anahitimisha Jaji huyo mkuu

View Comments