In Summary

Ugonjwa wa Sickle cell anemia ni ugonjwa wa damu ambao mtoto huzaliwa nao

Hupitishwa kupitia jeni za mzazi. Watoto walio na anemia ya seli mundu hufanya aina isiyo ya kawaida ya hemoglobin

Joy Watitwa
Image: Tony Wafula

HABARI NA TONY WAFULA;

Wagonjwa wa  anemia ya seli mundu kwa kimombo kama Sickle cell anemia katika Kaunti ya Bungoma wamelaumu wizara ya afya kwa kutowajali huku kukiwa na janga la Covid-19.

Ugonjwa wa Sickle cell anemia ni ugonjwa wa damu ambao mtoto huzaliwa nao.

Hupitishwa kupitia jeni za mzazi. Watoto walio na anemia ya seli mundu hufanya aina isiyo ya kawaida ya hemoglobin.

Hii ni protini katika seli nyekundu za damu ambayo hubeba oksijeni kwa sehemu zote za mwili. Kwa mgo jwa wa sickle cell anemia, viungo vya mwili na tishu hazipati oksijeni ya kutosha.

Joy Watitwa, 32, kutoka Kanduyi kaunti ya Bungoma alifichua kuwa amekuwa akipambana na sickle cell Anemia tangu kuzaliwa na kuongeza kuwa alipatikana akiwa na umri wa miaka 8.

Watitwa alisema kuwa safari yake ya kupambana na upungufu wa damu imekuwa ngumu huku akitoa wito kwa wazazi wenye watoto wenye ugonjwa wa sickle cell kuwapa uangalizi maalum na lishe bora ili waendelee kuishi.

"Watoto wanaokabiliana na anemia ya sickle cell wanapaswa kupewa uangalizi maalum, upatikanaji wa dawa na elimu," alisema, akiongeza kuwa watoto wa sickle cell ni werevy shuleni.

Bi.Watitwa alisema kuwa amekuwa akipambana na unyanyapaa na uonevu kutoka kwa wanafunzi wenzake kuanzia Shule ya Msingi hadi chuo kikuu, aliongeza kuwa licha ya changamoto hizo alifanikiwa kufaulu vizuri mitihani yake.

“Maisha yangu ya shule hayakuwa rahisi kwani nilikumbana na unyanyapaa kutoka kwa wanafunzi wenzangu ambao walikuwa wakinitelekeza kila nilipohitaji msaada, hata hivyo nilifanikiwa kupita na kufaulu vyema katika masomo yangu hadi ngazi ya chuo na kuhitimu Diploma ya Records management ," alisema.

Watitwa alidokeza kuwa gharama ya kumhudumia mgonjwa wa sickle cell ni ghali sana kwani kila tembe inagharimu zaidi ya Ksh.40 na mtu anahitaji angalau tembe mbili kwa siku.

Katika ombi lake, Watitwa aliiomba serikali kupitia wizara ya afya kuwazingatia wagonjwa wa sickle cell anemia na kuwajumuisha kwenye bima ya NHIF ili waweze kuokolewa.

“Nililipa milioni 1.8 katika hospitali ya Eldoret ambapo nilikuwa nikipokea matibabu ya sickle cell anemia  kwa sababu NHIF haikuwa ikiwahudumia wagonjwa wa sickle cell,” alisema.

Aliitaka serikali ya kaunti ya Bungoma kupitia wizara ya afya kuanzisha kituo cha seli mundu kitakachosaidia kuwatenga wagonjwa ambao wanaugua sickle cell anemia  haswa katika kipindi hiki cha Covid-19, akiongeza wagonjwa wengi wa sickle cell anemia wamepoteza maisha kutokana na ukosefu wa huduma za afya.

"Mgonjwa wa anemia hivi majuzi alifariki katika hospitali ya rufaa ya Kaunti ya Bungoma alipokuwa akisubiri dawa baada ya kuambukizwa Covid-19," alibainisha.

 

 

 

Joy Watitwa
Image: Tony Wafula
View Comments