In Summary
  • Uamuzi huo wa Jaji David Majanja ulifuatia ukaguzi wa Kamishna wa Kodi ya Ndani kuhusu masuala ya fedha
KIDERO-1

Mahakama Kuu imeamuru aliyekuwa Gavana wa Nairobi Evans Kidero alipe ushuru wa Sh427,269,795.

Uamuzi huo wa Jaji David Majanja ulifuatia ukaguzi wa Kamishna wa Kodi ya Ndani kuhusu masuala ya fedha na biashara ya gavana huyo wa zamani.

Licha ya gavana huyo wa zamani na Kamishna kufikia muafaka kwamba fedha zinazochangishwa kwa ajili ya kampeni za vyama vya siasa hazitozwi kodi, pande zote mbili zilishindwa kukubaliana iwapo Kidero, ambaye wakati huo alikuwa akigombea, kiti cha ugavana wa Nairobi, kilionyesha kwamba pesa zilizopatikana zimetumika katika kampeni za kisiasa.

 

 

View Comments