In Summary
  • Kuria, ambaye ni kiongozi wa Chama Cha Kazi, amekuwa asiyetabirika katika kuunda muungano wake wa 2022

Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria ameshikilia kuwa kambi ya Azimio La Umoja si chaguo kwake huku nchi ikielekea kwenye uchaguzi wa Agosti 9, mwaka huu.

Akizungumza katika Kaunti ya Kiambu mnamo Jumanne wakati wa mazishi ya mama ya aliyekuwa Gavana wa Kiambu Ferdinand Waititu, Kuria alisema atakuwa upande wa ushindi daima.

" Kuna kitu ninajua, pengine sijui pahali niliko lakini najua pahali siko," Kuria Alizungumza.

Kuria, ambaye ni kiongozi wa Chama Cha Kazi, amekuwa asiyetabirika katika kuunda muungano wake wa 2022.

"Unajua kwa hii uhai mimi ndio ninajiamulia, hakuna siku utanipata kwa Azimio…lakini hata nikikufa, msinipeleke kwa Azimio."

Hivi majuzi, Kuria alikutana na wakuu wa OKA na kusema walikuwa wamekubali kufanya kazi pamoja.

Alisema aliwafahamisha kuwa hatajiunga nao iwapo wataungana na Azimio.

Mbunge huyo alisema kuwa umaarufu wa Chama cha Jubilee katika eneo hilo utaisha hivi karibuni.

 

 

 

View Comments