In Summary
  • Seneta wa Makueni Mutula Kilonzo Junior ameonyesha nia ya kutaka kiti cha ugavana kuchukua nafasi ya Kibwana

Gavana wa Makueni Kivutha Kibwana ameonyesha nia ya kuwania kiti cha Seneti ya Makueni chini ya Chama cha Muungano katika uchaguzi wa Agosti 9.

Gavana huyo ambaye anahudumu muhula wake wa mwisho afisini alisema kuwa katika seneti kutamsaidia kulinda ugatuzi ipasavyo.

Alizungumza huko Makueni katika hafla ya Ijumaa, akisema kuwa wenyeji wamekuwa wakimsukuma kuwania useneta.

"Ninajua kwamba katika kule kusaidia devolution hapa kwetu kwa iyo kazi ya oversight…ninaweza kusaidia katika Senate kwa kazi ya ugavana nikijua kazi ya gavana ."

Pia alisema kuwa atakuwa katika nafasi ya kuongoza magurudumu ya ugatuzi nchini kote akiwa katika bunge la seneti.

“Sio kujivuna, iyo ni kitu ninajua. Ninajua pia vivyo kwa sababu nina wafadhili ambao nitawaletea gavana aendelee na kazi kwa sababu hata sasa nina mipango nyingi na wafadhili."

Seneta wa Makueni Mutula Kilonzo Junior ameonyesha nia ya kutaka kiti cha ugavana kuchukua nafasi ya Kibwana.

Muungano ni miongoni mwa vyama vilivyomuidhinisha kiongozi wa ODM Raila Odinga kuwania urais.

 

 

 

View Comments