In Summary

• Kabla ya uchaguzi mkuu wa Agosti 9, 2022, Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) ilikuwa imeruhusu mtu yeyote kuingia kwenye seva zao na kuyaona matokeo mwenyewe kwa kujihesabia.

NMG
Image: THE STAR//NMG

Shirika la habari la Nation baada ya kukumbwa na maswali mengi kwa kusitisha shughuli yao ya kuonesha jinsi uhesabu wa kura ulivyokuwa ukifanyika sasa wamesema walisitisha shughuli hiyo ili kupanga upya rasilimali ya kuwawezesha kujumulisha fomu 34B.

"National Media Group inaendelea kujumlisha na kuchapisha matokeo ya uchaguzi. Hata hivyo, uboreshaji wa matokeo ulipungua kutokana na upangaji upya wa rasilimali ili kujumlisha fomu 34B iliyotolewa tangu Ijumaa," taarifa hiyo ilieleza.

Kabla ya uchaguzi mkuu wa Agosti 9, 2022, Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) ilikuwa imeruhusu vyombo vya habari, vyama vya siasa, mashirika ya kiraia na umma kwa ujumla kufanya majumuisho yao ya matokeo ya uchaguzi, wahusika tofauti wamekusanya rasilimali kufanya hesabu kubwa katika kiini cha demokrasia ya Kenya.

Vyombo vya habari viliendelea na kuanzisha vituo vyao vya kuhesabia kura kuhesabu matokeo ya uchaguzi wa urais.

Ingawa wote walikuwa wanapata deta kutoka kwa tume ya uchaguzi, takwimu zilitofautiana katika vyombo vya habari kulingana na mambo kadhaa; kasi ya usindikaji wa data na wafanyikazi waliotumwa, jambo lililozua mkanganyiko miongoni mwa wakenya huku vituo vya runinga tofauti vikionesha takwimu tofauti na mgombea urais tofauti aliyekuwa anaongoza.

Taarifa ya NMG inakuja siku moja tu baada ya madai kuibuka kwamba seva za vituo vya runinga vilidukuliwa na watu waliojaribu kutamba na takwimu ila Ijumaa msimamizi wa kituo kikuu cha kuhesabu kura profesa Abdi Guliye alizungumzia suala hilo na kusema kwamab kulikuwepo na majaribio zaidi ya 200 ya kujaribu kudukuliwa kwa seva za IEBC ila hazikufanikiwa kwani timu yao ya utandawazi ilisimama tisti na kukomesha majaribio hayo.

View Comments