In Summary

“Kuanzia Septemba mosi, wateja wetu wa maeneo hayo wataendelea kupokea huduma zetu katika tawi la Village Market au matawi yaliyo karibu,” Safaricom ilitaarifu.

Duka la Safaricom Tawi la Two Riverws litafungwa mwisho Agosti 32 mwaka 2022.
Image: Facebook

Kampuni ya mawasiliano ya Safaricom imewatia Wakenya woga kuhusu hali ya uchumi nchini pamoja na mazingira ya kibiashara baada ya kutangaza kwamba wanafunga duka lao lililopo katika maeneo ya Two Rivers jijini Nairobi.

Kupitia ukurasa wao rasmi wa Faceook, kampuni hiyo kubwa kabisa ya mawasiliano nchini katika kile watu wengi wamesema ni nadra kutokea kwao ilitoa taarifa ya kusitisha kutoa huduma katika tawi lao lililopo maeneo hayo kuanzia Septemba tarehe moja.

“Kama ambavyo tunaendelea kuboresha huduma zetu ili kuafikia na bora kukimu mahitaji ya wateja wetu, tungependa kuwajulisha wateja wetu kuhusu kufungwa kwa tawi letu la Two Rivers kuanzia mwisho kabisa wa siku ya tarehe 31 Agosti mwaka huu,” Safaricom walitangaza.

Pia waliwasihi wateja wao karibu na eneo hilo na ambao walikuwa wanategemea huduma zao kutoka tawi la Two Rivers kutojali na kuendelea kupata huduma hizo kutoka tawi la karibu lililopo Village Market.

“Kuanzia Septemba mosi, wateja wetu wa maeneo hayo wataendelea kupokea huduma zetu katika tawi la Village Market au matawi yaliyo karibu,” Safaricom ilitaarifu.

Taarifa ya Safaricom kufunga moja ya matawi yake ilipokelewa kwa mshtuko mkubwa na wateja wa kampuni hiyo kwani wengi huwa wanaiona kama moja ya kampuni zilizostawi sana nchini kutokana na faida kubwa wanayoitengeneza kutoka kwa mamilioni ya wateja wanaopendelea huduma zao.

Wengine walisaili kutaka kujua kama ni hali mbaya ya uchumi au ni mazingira ambayo yamegeuza mawimbi dhidi ya kampuni hiyo huku wengine wakisema kwamba Safaricom ni kama inaanguka na kutia wasiwasi katika biashara nyingi ambazo zinaitegemea kampuni hiyo si tu kwa huduma za simu bali pia katika kufanya biashara ya kuuza na kununua mtandaoni.

“Ni kubaya kama ata Safaricom inapunguza kasi. Utawala mbaya zaidi tangu uhuru,” mmoja kwa jina Ndúmia Nkwire Cíonthe alitoa maoni katika ukurasa huo.

Hali ya uchumi nchini nazidi kudorora huku biashara nyingi haswa zile za chini zikiendelea kuathirika mno kutokana na gharama kubwa ya kununua bidhaa za jumla ili kuuzia watumiaji kwa bei ya reja reja.

View Comments