In Summary

• Chama cha ODM kiliwateua Irene Mayaka na John Ngongo kuwakilisha wafanyikazi huku Umulkher Mohamed aliteuliwa kuwakilisha vijana.

Bunge
Image: Maktaba

Serikali imechapisha orodha ya viongozi wote walioteuliwa kushikilia nyadhifa mbali mbali kwenye mabunge ya kitaifa na lile la seneti.

Kutoka chama cha UDA, Jackson Kosgei ameteuliwa kuwakilisha watu wenye ulemavu, Teresia Mwangi kuwakilisha vijana, Abdisirati Ali kuwakilisha kundi la watu waliotengwa, Dorothy Ikiara na Joseph Iraya wakiteuliwa kuwakilisha wafanyikazi kwenye bunge la kitaifa.

Suleka Halum ameteuliwa kuwakilisha wanawake.

Kutoka chama cha ANC, Joseph Denar ameteuliwa kuwakilisha wafanyikazi wa jamii.

Chama cha ODM kiliwateua Irene Mayaka na John Mbadi kuwakilisha wafanyikazi huku Umulkher Mohamed aliteuliwa kuwakilisha vijana.

Jubilee kilimteua aliyekuwa mwakilishi wa kike wa Murang’a Sabina Chege kuwakilisha wanawake huku Wiper wakiwa bado wamezuiliwa kufanya uteuzi kutokana na kesi iliyopo kortini.

Katika orodha ya wanawake walioteuliwa kuwakilisha katika bunge la seneti, chama cha UDA kiliorodhesha Veronica Nduati, Roselinda Tuya, Miraj Abdulrahman, Gloria Orwoba, Joyce Korir, Karen Nyamu, Peris Tobiko, Miriam Omar, na Maureen Mutinda.

Katika kitengo hicho, ODM waliteua Catherine Mumma, Beatrice Oyomo, Hamida Kibwana, Betty Montet, na Beth Syengo. Margaret Kamar aliteuliwa na Jubilee huku Shakilla Mohamed akiteuliwa na Wiper.

Hezena Lemaletian wa ODM na Raphael Mwinzagu wa UDA waliteuliwa Kwenda Seneti kuwakilisha vijana huku Crystal Asige wa ODM na George Mbugua wa UDA wakiteuliwa Kwenda bunge hilo  la seneti kuwakilisha watu wenye ulemavu.

View Comments