In Summary

• Elizabeth, alichukuwa usukani wa ufalme akiwa kwenye ziara nchini Kenya mwezi Februari 1952 alipopokea habari za kifo cha babake.

Uhuruto

Rais Uhuru Kenyatta na Rais mteule William Ruto wameungana na viongozi wengine wa dunia kuomboleza kifo cha Malkia Elizabeth II. 

Malkia alifariki siku ya Alhamisi katika Kasri lake la Balmoral huko Aberdeenshire, Scotland.

 Uhuru, katika ujumbe wake wa rambirambi kwa Mfalme Charles III, Familia ya Kifalme, Waziri Mkuu Liz Truss na watu wa Uingereza, aliomboleza malkia huyo aliyekuwa na umri wa miaka 96 kama kielelezo cha kimataifa cha utumishi usio na ubinafsi kwa ubinadamu. 

"Malkia Elizabeth II alikuwa mnara wa huduma ya kujitolea kwa binadamu na kiongozi mkuu wa Uingereza, mataifa ya Jumuiya ya Madola, ambapo Kenya ni mwanachama na ulimwengu mzima," alisema. 

Uhuru alisema alipokea habari za kusikitisha za kifo cha Malkia Elizabeth II kwa huzuni na hisia kubwa.

Ruto alisema uongozi wa malkia ulikuwa jambo la kuzingatia.

“Tutakosa uhusiano mzuri aliofurahia na Kenya na kumbukumbu zake ziendelee kututia moyo. Tunaungana na Jumuiya ya Madola katika maombolezo na tunatoa rambirambi kwa Familia ya Kifalme na Uingereza,” alisema.

"Kumbukumbu zake ziendelee kututia moyo. Tunaungana na Jumuiya ya Madola katika maombolezo na tunatoa rambirambi kwa Familia ya Kifalme na Uingereza," alisema Ruto.

"Aliongoza mageuzi ya taasisi hiyo kuwa jukwaa la ushirikiano mzuri wa kimataifa," Ruto alisema kwenye Twitter Alhamisi usiku, akielezea umoja huo kama ushuhuda wa "urithi wa kihistoria" wa Malkia.

Elizabeth, alichukuwa usukani wa ufalme akiwa kwenye ziara nchini Kenya mwezi Februari 1952 alipopokea habari za kifo cha babake alipokuwa akiishi katika hoteli ya Treetops, lodge iliyoko ndani ya msitu wa Aberdare.

Kenya, ambayo wakati huo ilikuwa koloni la Uingereza, ilikuwa kituo cha kwanza katika ziara ya Jumuiya ya Madola ambayo alikuwa ameanza na mumewe, Prince Philip, badala ya baba yake mgonjwa.

Ulikuwa usiku katika hoteli ya Treetops ambapo Elizabeth alibadilika kutoka Binti wa kifalme na kuwa Malkia.

View Comments