In Summary

• Ajali hiyo ilitokea asubuhi ya Jumamosi na mpaka ashuhuri bado shughuli zilikuwa zimetatizika kwenye barabara hiyo.

Asubuhi ya Jumamosi kulikuwwepo na klipu moja inayoonesha gari moshi likiwa limepoteza mweleko kwenye njia kuu ya reli na kuanguka maeneo ya Kakamega Magharibi mwa Kenya.

Kulingana na taarifa zilizochapishwa Twitter na ukurasa wa Ma3 Route, gari la moshi lilikuwa njiani kuelekea jiji la Kisumu mwendo was aa tatu asubuhi ajali hiyo ndogo ulipotokea.

Ajali hiyo ilitokea baada ya sehemu ya mbele ya treni hiyo kuacha reli na kupinduka kiasi cha kilomita chache hadi stesheni inayoziba barabara ya Kakamega Kisumu.

Abiria walilazimika kushuka kutoka kwa treni hiyo baada ya kusimamishwa, lakini hakukuwa na majeruhi, na madereva waliokuwa wakisafiri katika barabara ya Kisumu - Kakamega walilazimika kutumia njia mbadala.

Hata hivyo, hakukuwa na majeruhi. Kulingana na habari hizo zilizochapishwa Twitter. Wakaazi walipigwa na kishindo na hawakujua ni nini kilikuwa kimetokea, na kugundua kuwa ilikuwa treni.

Shirika la reli nchini lilitoa taarifa hizo na kusema kwamba ajali hiyo ilitokana na kujaa matope katika sehemu hiyo ya reli ambapo ni makutano ya barabara ya Kisumu kuelekea Kakamega.

Shirika hilo limelaumu hali mbovu ya mifereji ya maji sehemu hiyo kuwa ndio ilichangia kujaa kwa matope yaliyopoteza mwelekeo wa garimoshi.

“Tungependa kuwataarifu umma kwamba hakukuwa na majeruhi yoyote katika mabohari ya treni yaliyoathirika. Tunaendelea kufanya kazi kwa ushirikiano wa karibu na shirika la KeNHA ili kupunguza msongamano katika barabara uliosababishwa na kuanguka kwa treni ili kurejesha hali kawaida. Watumizi wa barabara wanataarifiwa kutumia barabara mbadala kwa muda huu,” Kenya Railways waliripoti.

View Comments