logo

NOW ON AIR

Listen in Live

IPOA yalaani shambulio la ujambazi la Turkana lililosababisha vifo vya watu 11

Shambulizi hilo lilitokea katika Kijiji cha Namariat katika Kaunti ya Turkana.

image
na Radio Jambo

Habari26 September 2022 - 18:41

Muhtasari


  • Alisema kuwa wameanzisha zoezi la kufuatilia mashambulizi ya Turkana kama walivyofanya kwa mashambulizi ya Mpeketoni na Kapedo

Mamlaka Huru ya Kusimamia Polisi (IPOA) imelaani shambulio la ujambazi la Turkana lililosababisha vifo vya maafisa 10 wa utawala na raia siku ya Jumamosi.

Shambulizi hilo lilitokea katika Kijiji cha Namariat katika Kaunti ya Turkana.

Katika taarifa siku ya Jumatatu, mwenyekiti wa IPOA Anne Makori alisema watafuatilia na kutoa mapendekezo kuhusu shambulio hilo.

"Kwa nchi yoyote, kupoteza maafisa wa usalama na wananchi kupitia vitendo vya uhalifu ni suala la kutia wasiwasi mkubwa," Makori alisema.

 

"Ni matumaini yetu kwamba kutakuwa na hatua madhubuti za uongozi wa polisi kulingana na uzito wa uhalifu uliofanyika katika kijiji cha Namariat."

Alisema kuwa wameanzisha zoezi la kufuatilia mashambulizi ya Turkana kama walivyofanya kwa mashambulizi ya Mpeketoni na Kapedo.

Zoezi la ufuatiliaji litaongozwa na Kurugenzi ya Ukaguzi, Utafiti na Ufuatiliaji ili kubaini mazingira ya shambulio la Turkana.

Makori alisema iwapo ufuatiliaji huo utatekelezwa kikamilifu, utasaidia katika kupunguza changamoto za usalama nchini Kenya.

"Hii ni sawa na kupinga mamlaka ya Kenya na inataka jibu thabiti lakini halali la polisi ili kuhakikisha amani idumu kote nchini," Makori alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved