In Summary
  • Mbunge huyo alitajwa miongoni mwa mawaziri 22 waliopendekezwa na Rais William Ruto waliomwona anafaa kuongoza katika afisi hiyo

Mbunge wa Garissa Mjini Aden Duale hamemsshukuru rais Ruto baada ya kuteuliwa kuwa waziri wa Ulinzi katika baraza la mawaziri siku ya Jumanne.

Mbunge huyo alitajwa miongoni mwa mawaziri 22 waliopendekezwa na Rais William Ruto waliomwona anafaa kuongoza katika afisi hiyo.

"Asante bosi wangu, Rafiki yangu na Rais wangu William Ruto. Leo alasiri nilipokea habari za kuteuliwa kwangu kama waziri wa ulinzi ajaye kwa heshima, furaha na unyenyekevu," akasema.

"Kwa hakika nimenyenyekea kwa fursa ya kutumikia watu wa Kenya kama katibu wa baraza la mawaziri la Ulinzi. Ninakushukuru Rais wangu kwa imani yako katika uongozi wangu na kwa kunipa fursa hii adhimu."

Kiongozi huyo wa zamani wa wengi alisimulia jinsi alivyoanza safari yake na Rais.

"Hakika, njia zetu na wewe Mheshimiwa zilikutana mwaka wa 2007 na tangu wakati huo nyota zetu zimeng'aa zaidi na zaidi," alisema.

Duale alisema Ruto amemsaidia sana katika safari yake ya kisiasa na hawezi kumshukuru vya kutosha.

“Tulianza safari yetu ya kuwatumikia wananchi kwa pamoja mwaka 2007 na kupitia wewe Rais wangu niliteuliwa kuwa Waziri wa Mifugo katika Serikali Kuu ya Muungano,” alisema.

Duale amekuwa mfuasi mkuu na mshirika wa Rais kwa miaka mingi, sifa ambayo ilimfanya kuteuliwa kuwa Kiongozi wa Wengi wa Wengi katika utawala wa Jubilee mnamo 2013.

Hii ilikuwa baada ya chama cha URP cha Ruto kuungana na TNA cha Rais wa zamani Uhuru Kenyatta kuunda serikali mpya.

 

 

 

 

View Comments