logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwili wa ajuza wa miaka 90 wapatikana kichakani ukiwa uchi

Mwili wa marehemu ulipatikana kichakani ukiwa hauna nguo.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri03 October 2022 - 13:44

Muhtasari


• Mwili wa ajuza huyo wa miaka 90 ulipatikana jioni ya Alhamisi, Septemba 29, 2022, na mwili wake kugunduliwa Jumapili jioni Oktoba 2.

• Mwili wa ajuza huyo ulipotea kwa siku 3 alipoenda kupalilia mimea shambani.

crime scene

Ajuza wa miaka 90 kutoka kijiji cha Kiandugira kaunti ya Murang'a ambaye alipotea kwa siku 3 hatimaye mwili wake ulipatikana ukiwa umetupwa katika kichaka huku ukiwa uchi wa hayawani Septemba 29.

Kulingana na mtu mmoja wa familia alithibitisha ajuza huyo alienda shambani ambako alikuwa akipalilia mimea yake lakini hakurejea nyumbani.

Mwili wake ulipatikana jioni ya Alhamisi, Septemba 29, 2022, na mwili wake kugunduliwa Jumapili jioni Oktoba 2 akiwa uchi na mwenye majeraha kana kwamba alidhulumiwa kabla ya kuuawa.

"Alikuwa uchi, alikuwa na majeraha kadhaa na inaonekana kama wahalifu walikuwa wamembaka kabla ya kumuua," Mwanafamilia alielezea kituo kimoja cha runinga humu nchini.

Watu wa familia walisema walipatwa na wasisiwasi giza lilipoingi bila ya nyanya yao kurudi. Shughuli za kumtafuta zilianza bila kuzaa matunda.

"Tulifanya mchakato wa kukwangua eneo hilo tukimtafuta lakini hatukumpata," mmoja wa familia alieleza.

Familia ilipata mshtuko baada ya kufahamishwa kuwa jamaa yao alikuwa ameuawa kwa mauaji ya kikatili na mwili wake kutupwa kwenye kichaka.

Sasa familia hiyo inalilia serikali iwahakikishie haki itatendeka na wahalifu waliotekeleza tendo hilo la kinyama wametiwa mikononi mwa sheria.

"Hatujui ni nani angeweza kufanya kitendo kiovu kama hiki lakini tunaomba uchunguzi ufanyike haraka ili washukiwa hao wahukumiwe," alisema.

Wakazi hao wamelaani tukio hilo la kusikitisha huku wakilihusisha na ongezeko la matumizi ya dawa za kulevya katika eneo hilo wakidai kitendo hicho kinaweza kufanywa na waraibu hao.

"Hakuna mtu mwenye akili timamu ambaye angefanya kitendo kama hicho kumshambulia mwanamke mzee, kumbaka na kumuua," mkaazi mmoja alielezea kituo kimoja cha habari humu nchini.

“Tunawaomba polisi kuharakisha uchunguzi na kuwakamata waliohusika na mauaji haya,” mkaazi huyo  liongeza .


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved