In Summary
  • Akizungumza kwenye sherehe za Siku ya Mashujaa siku ya Alhamisi, Ruto alibainisha kuwa taasisi hizo zikiwemo sekta ya haki, sheria na utaratibu hazitahujumiwa
WILLIAM RUTO Rais wa tano wa Kenya
Image: Facebook//WILLIAMRUTO

Rais William Ruto kwa mara nyingine tena ameapa kulinda uhuru wa taasisi huru.

Alisema chini ya utawala wake hakutakuwa na kuingiliwa au jaribio lolote la kudhibiti, kuelekeza taasisi zinazojitegemea.

Akizungumza kwenye sherehe za Siku ya Mashujaa siku ya Alhamisi, Ruto alibainisha kuwa taasisi hizo zikiwemo sekta ya haki, sheria na utaratibu hazitahujumiwa.

"Watatekeleza majukumu yao kwa uhuru na weledi na vivyo hivyo kusimamiwa na vyombo vinavyofaa. Hii ni dira yetu katika kuhakikisha kwamba njia ya rushwa yenyewe haiharibiwi na uingiliaji kati usiofaa," alisema.

Aliendelea zaidi na kuongeza kuwa ni sharti wafanyikazi wa umma wawajibikie matendo yao ili kufanya taasisi ziendeshwe vyema.

"Vita dhidi ya ufisadi lazima vishinde. Serikali yetu inakusudia kuendeleza vita hivi na kuonyesha dhamira yake ya kutovumilia rushwa."

Pia Rais William Ruto katika hotuba ya kwanza kabisa katika sherehe ya kwanza ya kitaifa kwenye uongozi wake, ilikuwa ni hotuba yenye wingi wa matumaini na ahadi tele zinazonuiwa katika kukomoa taifa hili kutoka mporomoko wa uchumi na kupanda kwa gharama ya maisha.

Rais Ruto alielezea mpango wa serikali yake katika kuboresha usalama wa chakula nchini Kenya ambapo alidokeza kwamba serikali itashirikiana na mashirika ya kininafsi ili kujenga mabwawa kadhaa ambayo yataweka maji kwa ajili ya unyunyiziaji mashamba ya kukuza vyakula.

Rais alisema kwamba njia pekee ya kupata suluhu la muda mrefu katika kukomesha njaa ni kuhakikisha kwamba kiangazi kinafutiliwa mbali kwa kuhakikisha maji yanapatikana kwa wingi ili kukuza vyakula na kupunguza bei ya vyakula ambayo sasa imepanda kwa kasi ya ajabu.

 

 

View Comments