In Summary

• Muganda alikuwa afisa mchapakazi, aliyejituma na aliyejitolea ambaye alitekeleza majukumu yake vyema na alishirikiana vyema na wenzake - DCI waliomboleza.

DCI Wamuomboleza afisa wao mbunifu
Image: Facebook//DCI

Kitengo cha polisi wa upelelezi wa jinai na uhalifu DCI wanaomboleza kifo cha mbunifu wao mkuu ambaye alikuwa anabuni picha na michoro ya kelezea matuko kupitia picha.

 

Kulingana na taarifa zilizochapishwa kwenye ukurasa wa Facebook wa DCI, afisa huyo kwa jina Boniface Mugenda aligongwa na pikipiki iliyokuwa ikiendeshwa kwa kasi na kupoteza maisha papo hapo.

 

“Kitengo cha Upelelezi wa Makosa ya Jinai kinaomboleza kifo cha mbunifu mkuu Boniface Muganda, ambaye aligongwa na mwendesha pikipiki aliyekuwa akiendesha mwendo kasi jana usiku kwenye barabara ya basi ya Northern By-Passsehemu ya Marurui, karibu na klabu ya Ashaki,” DCI waliomboleza.

Muganda ambaye ni mfanyakazi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Biashara na Masuala ya Umma alikuwa anaelekea nyumbani kwa pikipiki yake wakati mwendesha pikipiki mwingine alimgonga na kuondoka huku akimwacha afisa huyo akiwa ameanguka barabarani.

Kulingana na wasamaria wema waliofika eneo la tukio, walimkimbiza hospitali ya chuo cha Kenyatta lakini kwa bahati mbaya alifariki hata kabla ya kuhudumiwa.

“Muganda alikuwa afisa mchapakazi, aliyejituma na aliyejitolea ambaye alitekeleza majukumu yake vyema na alishirikiana vyema na wenzake kutoka idata zote. Alikuwa Afisa Mawasiliano mwenye kipawa ambaye ujuzi wake katika picha, videografia na usanifu wa michoro ulimsukuma kusimamia dawati la ubunifu katika kitengo cha mawasiliano cha DCI,” walimsifia marehemu.

Afisa huyo wa upelelezi ambaye amewahi kuhudumu katika kitengo cha uchunguzi wa picha na acoustics alikuwa msanii mbunifu katika toleo la hivi punde la Jarida la DCI miongoni mwa majukumu mengine ikiwa ni pamoja na kuangazia maadhimisho ya siku ya Mashujaa ya Alhamisi iliyopita katika bustani ya Uhuru.

View Comments