In Summary
  • Akiongea Jumatatu katika mazishi huko Mumias, Odinga alishangaa ni kwa nini watu wengine serikalini kesi zao zifutiliwe mbali ilhali Waluke ameachwa gerezani
Raila Odinga
Image: RAILA ODINGA/TWITTER

Kinara wa Azimio one Kenya Raila Odinga ametaka kuachiliwa kwa mbunge wa Sirisia John Waluke ambaye aliamriwa kulipa faini ya Ksh.1 bilioni au kutumikia kifungo cha miaka 67.

Akiongea Jumatatu katika mazishi huko Mumias, Odinga alishangaa ni kwa nini watu wengine serikalini kesi zao zifutiliwe mbali ilhali Waluke ameachwa gerezani.

"Sasa suala lingine, watu walioshtakiwa kwa mauaji wanasamehewa na kuidhinishwa kuwa  mawaziri, wengine wenye kesi za ufisadi wa mabilioni wanaachwa huru. Kwa upande mwingine, watu wetu wananyanyaswa. Kesi ya Mbunge wa Sirisia Waluke ni suala la kiraia,” alisema Odinga.

Kiongozi huyo wa Azimio alidai kuwa si haki kwa Waluke, katika umri wake, kupewa hukumu kama hiyo katika kesi yake.

"Yeye (Waluke) amehukumiwa kifungo cha miaka 67 gerezani lakini tayari ana zaidi ya miaka 60. Ni kama kunifunga jela miaka 50. Unawaachilia watu kama Linturi, Gachagua na mwanamke mwingine kisha kumfunga Waluke. Je, hiyo ni haki? Tunataka Waluke apewe bondi kisha kesi itupiliwe mbali," alisema Odinga.

 

 

 

 

View Comments