logo

NOW ON AIR

Listen in Live

''Hili ni jengo la 8 kuporomoka Kiambu katika miezi 6 Kiambu'' - Gavana Wamatangi

Kimani wamatangi alisema maeneo mengine majengo yalibomoka ni kama vile Kinoo,Ruiru na Kirigiti

image
na Davis Ojiambo

Habari17 November 2022 - 13:00

Muhtasari


  • • Wamatangi alisema huenda ikawa huo ni mkasa 8  ambao imeboromoka chini ya nusu mwaka.
  • • Wa 3 walifariki na wengine kadhaa kuokolewa kutoka kwa jengo liliporomoka eneo la Ruaka Kiambu.
Gavana wa Kiambu Kimani Wa Matangi

Gavana wa Kiambu Kimani Wamatangi siku ya Alhamisi alisema kwamba kisa cha hivi punde cha jengo kuporomka Ruaka ni cha nane katika kaunti ya kiambu kwa kipindi cha chini ya miezi sita.

Aliyataja maeneo kama Kasarani, Kinoo na Ruiru ambayo yameshuhudia visa vya hivi punde vya majengo kuporomoka. 

Mbali na hayo Wamatangi alisema atamenyana na wamiliki wa nyumba ambao hawafuati sheria zilizowekwa na  halmashauri ya ujenzi nchini NCA. 

Kulingana na Gavana Kimani Wa Matangi agizo lilikuwa limetolewa kusitisha ujenzi wa  jengo hilo ila wasimamizi walipuuzilia.

''Hilo jengo lilikuwa limepigwa marufuku tangu mwezi wa Mei 2022 na mara nyingi wameshikwa na maafisa wa polisi na wakiachiliwa wanarudi kwenye ujenzi''  Wamatangi alisema.

Aliahidi kuandaa kikao cha haraka na mamlaka ya kusimamia ujenzi NCI kujaribu kupata suluhu ya kudumu na kuhakikisha mtu yeyote anaye endeleza ujenzi bila idhini wala stakabathi zinazofaa achukuliwe hatua mara moja.'


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved