logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwanafunzi mkongwe duniani afariki akiwa na miaka 99 akiwa darasa la 7

Atakumbukwa kwa jinsi alivyoyatilia masomo yake thamani licha ya umri wake  mkongwe.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri18 November 2022 - 05:10

Muhtasari


• Sitienei alikuwa anasomea shule ya Vision Preparatory iliyoko Ndalat kaunti ya Nandi.

• Alianza kusoma akiwa na umri wa miaka 89 hadi kifo chake.

Sitienei akiwa darasani.

Familia ya mwanafunzi anayeaminika kuwa mkongwe zaidi duniani ilithibitisha kifo chake, alifariki akiwa na umri wa miaka 99.

Mwanafunzi huyo Gogo Priscilla Sitienei alizua gumzo mitandaoni baada yake kujiunga na shule ya Vision Preparatory iliyoko Ndalat kaunti ya Nandi miaka 11 iliyopita kwa ajili ya masomo.

Sitiene aliyekuwa mwanafunzi wa darasa la 7 alijizolea umaarufu huu wakati aliposhiriki kwenye filamu ya kifaransa iitwayo ‘Gogo Priscilla’ mwaka wa 2021.

Sammy Chepsiror , mjukuu wake alisema nyanya yao alifariki kwa amani nyumbani kwake.

“Nyanya alikuwa na afya njema na alihudhuria masomo yake. Hata hivyo, hivi majuzi, alianza kulalamikia maumivu ya kifua, jambo ambalo kukosa kuhudhulia shule,” alisema mjukuu huyo.

Alisema kifo chake kilitokana na matatiza yanayohusiana na umri na wiki ya kifo chake alizidiwa na hali mbaya ya afya na kufariki kwa amani akiwa usingizini.

Sitienei  atakuwa wa kuigwa sio tu Marekani bali humu nchini kwa jitihada za kuwasaidia wanawake wajawazito kama mkunga wa jadi na kisha kuazisha elimu akiwa a umri wa miaka 89.

Gavana wa Nandi Stephen Sang alikuwa miongoni mwa viongozi waliotoa rambirambi zao kwa familia huku wakimuenzi na kummiminia sifa kedekede Sitienei kama mtu aliyekuwa na ari kubwa masomoni.

 

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved