In Summary
  • Kufikia sasa, visa 160 vya kipindupindu vimerekodiwa katika jiji kuu huku wizara ikisema kuwa jumla ya visa 13 vinaambukizwa kutoka nje

Watu wanane wamefariki jijini Nairobi kutokana na mkurupuko wa kipindupindu, Wizara ya Afya imesema.

Sita walikufa hospitalini huku vifo viwili vikitokea katika jamii.

Kulingana na taarifa ya wizara hiyo, kaunti ndogo ya Embakasi Mashariki ndiyo iliyoathiriwa zaidi na mkurupuko huo huku eneo hilo likirekodi visa vinne katika muda wa saa 24 pekee.

Kufikia sasa, visa 160 vya kipindupindu vimerekodiwa katika jiji kuu huku wizara ikisema kuwa jumla ya visa 13 vinaambukizwa kutoka nje.

Kutokana na takwimu, 91 ni wanaume huku 69 ni wanawake.

"Wanaume zaidi ikilinganishwa na wanawake wameathiriwa na kipindupindu, huku jamii ya umri wa miaka 21 hadi 30 ikiwa imeathiriwa zaidi leo, ikifuatiwa na miaka 51-60," wizara hiyo inasema.

Kipindupindu ni ugonjwa wa kuhara unaosababishwa na maambukizi ya bakteria ya Vibrio cholerae kwenye utumbo.

 

 

 

 

View Comments