In Summary
  • "Kuna shule tunapata waombaji wengi lakini uwezo ni mdogo hivyo haiwezekani watahiniwa wote kupangiwa shule za ndoto zao
WAZIRI WA ELIMU EZEKIEL MACHOGU
Image: ANDREW KASUKU

Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu mnamo Jumatatu, Januari 16, aliorodhesha shule kumi zilizopokea idadi kubwa zaidi ya maombi zaidi ya uwezo wao.

Akizungumza nje ya Taasisi ya Ukuzaji Mtaala ya Kenya (KICD), Waziri huyo aliangazia shule bora zaidi kama vile Shule ya Upili ya Kabianga, shule ya upili ya Nakuru, shule ya upili ya Nanyuki, na Shule ya Wasichana ya Alliance miongoni mwa zingine.

Hata hivyo, alidokeza kuwa zoezi la upangaji wa nafasi hizo lilionyesha kuwa watahiniwa wengi hawakuongozwa ipasavyo na wakuu wao wa shule na walimu.

"Wakati wa mchujo, ilidhihirika kuwa idadi kubwa ya watahiniwa hawakupata mwongozo unaofaa wakati wa kuchagua shule. Haya yalisababisha baadhi ya shule kupata waombaji wengi dhidi ya uwezo wao. Hakuna mtu atakayeweza kwenda nje ya uwezo," alisema.

"Kuna shule tunapata waombaji wengi lakini uwezo ni mdogo hivyo haiwezekani watahiniwa wote kupangiwa shule za ndoto zao," aliongeza.

Waziri wa Elimu alithibitisha kuwa muda wa kuripoti kwa watahiniwa wa KCPE utakuwa kuanzia Februari 6, 2023 hadi Februari 13, 2023.

Hizi hapa baadhi ya shule hizo;

1.Shule ya wasichana ya Butere

2.Shule ya wavulana ya Kapsabet

3.Shule ya upili ya Mang'u

4.Shule ya upili ya Nakuru

5.Shule ya wasichana ya Alliance

6.Shule ya upili ya Nyandarua

7.Shule ya upili ya Maeno

8.Shule ya upili ya Kabianga

9.Shule ya pili ya Pangani

10.Shule ya upili ya Nanyuki

 

 

 

 

View Comments