In Summary
  • "Nilienda nyumbani kwangu na nilikuwa huko siku zote, sikwenda kujificha popote," alisema.
Aliyekuwa mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati
Image: DOUGLAS OKIDDY

Aliyekuwa mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati amesema hakuwahi kujificha baada ya kutangazwa kwa matokeo ya mwisho ya urais mnamo Agosti 15 mwaka jana.

Chebukati ambaye alikuwa akijibu maswali ya wakili Donald Kipkorir anayemwakilisha kamishna aliyesimamishwa kazi Irene Masit alisema alikuwa katika makazi yake.

Kipkorir alitaka kujua ikiwa pia alijificha kama makamishna wengine wawili wa zamani Abdi Guliye na Boya Molu waliodai walilazimikakujificha kwa siku tatu.

"Nilienda nyumbani kwangu na nilikuwa huko siku zote, sikwenda kujificha popote," alisema.

Akitoa ufichuzi wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Tathmini ya baada ya uchaguzi wa 2022 katika Safari Park jijini Nairobi mnamo Januari 16, Guliye alisema matukio ya siku hiyo ya kutisha yalikuwa ya kuogofya.

Alisema pamoja na Molu na Mkurugenzi Mtendaji, Marjan Hussein walikwenda kusikojulikana na kurejea baada ya mambo kutulia.

"Baada ya tangazo la Bomas la matokeo ya urais, nakumbuka nikienda Siberia katika kaunti yangu pamoja na Mkurugenzi Mtendaji Marjan na kamishna Molu, tulijificha, tukazima simu zetu kwwa siku tatu,'alisema.

Akizungumza mbele ya jopo kazi siku ya Jumanne, Chebukati alisema makamishna walikuwa wamekubaliana kuwa kamishna Abdi Guliye ndiye atangaze matokeo hayo.

Alisema kuwa Guliye alipangwa kutangaza matokeo kabla ya yeye kutoa tangazo la mwisho kuhusu matokeo ya mwisho ya urais.

Chebukati alisema matokeo hayo hayakutangazwa kwa sababu ghasia ilizuka katika ukumbi huo.

View Comments