In Summary
  • Watano hao pia walizaliwa kabla ya wakati mama yao - Margaret Wairimu- alipata uchungu akiwa na miezi saba

Msimamizi wa Matibabu wa Hospitali ya Nakuru Level Five Dkt Aisha Maina alieleza kuwa watoto watano waliozaliwa katika Kaunti ya Nakuru mnamo Jumatano, Februari 1, walikuwa na nafasi ndogo ya kunusurika kwa vile walikuwa na uzito mdogo.

Akizungumza na TV47, daktari huyo aliongeza kuwa viungo vya ndani vya watoto hao havikuwa vumekua kikamilifu kutokana na uzito wao.

Kulingana na hospitali hiyo, watoto hao wachanga walikuwa na uzito wa kati ya gramu 500 na 650.

Watano hao pia walizaliwa kabla ya wakati mama yao - Margaret Wairimu- alipata uchungu akiwa na miezi saba.

Hii iliwalazimu madaktari katika kituo hicho kuwaweka wasichana hao wanne na mvulana kwenye mashine baada ya kuzaliwa.

Walakini, mnamo Alhamisi, Februari 5, saa 24 tu baada ya kuzaliwa, watoto wachanga walithibitishwa kufariki.

“Alilazwa (mama) mara moja na kuwekwa chini ya uangalizi wa wataalamu hadi alipopata uchungu na kufanyiwa upasuaji wa dharura.

"Kwa sababu ujauzito ulikuwa wa miezi saba, watoto walizaliwa na uzito mdogo sana," daktari alisema wakati huo.

Kuzaliwa kwa watoto hao watano kuligonga vichwa vya habari Jumatano baada ya baba yao, Simon Ndung'u - dereva wa matatu, kuwasihi Wakenya msaada.

“Ninawaomba wasamaria wema kuniunga mkono. Uchunguzi wake wa hivi majuzi ulionyesha kwamba alikuwa amebeba watoto watatu lakini wengine wawili walizaliwa wakati wa kuzaliwa,” baba huyo alizungumza siku ya Jumatano.

View Comments