In Summary
  • Aidha Natembeya alisema kaunti itashirikiana na tume ya huduma ya Walimu na Wizara ya Elimu ili kuhakikisha sekta ya elimu nchini Trans Nzoia inaendeshwa kwa ufanisi
gavana george natembeya
Image: hisani

Gavana wa Trans Nzoia George Natembeya alisema ametenga Sh120 milioni kugharamia karo za shule za wanafunzi wasio na uwezo katika kaunti hiyo.

Akizungumza katika KBC Jumatano, alisema fedha hizo zimetengewa wanafunzi wasiojiweza katika kaunti hiyo waliopata zaidi ya alama 250 katika KCPE.

Natembeya alisema mpango huo ulioanzishwa na serikali ya kaunti hautakuwa wa mara moja tu.

Alisema utafanyika kwa miaka mingi huku ufadhili ukitengwa katika kila mwaka wa fedha ili kuhakikisha mpango huo unafanikiwa.

“Tumetenga Sh120 milioni mwaka huu wa fedha na tutakuwa tukifanya hivyo kila mwaka. Kufikia wakati tunafanya mwaka wetu wa nne tutakuwa tumetenga takriban shilingi milioni 400 kutatua tatizo hili,” Natembeya alisema.

Alisema wanafunzi kutoka familia zisizo na uwezo ambao wamepangiwa kujiunga na shule za upili katika kaunti hiyo watagharamiwa kwa miaka minne na serikali ya kaunti.

"Tumeazimia kama kaunti kuwalipia karo watoto wetu wote waliopata alama zaidi ya 250 ambao wamekubaliwa katika shule za kutwa na kutoka kwa familia zenye uhitaji. Tunakwenda kulipa ada kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne,” alisema.

Aidha Natembeya alisema kaunti itashirikiana na tume ya huduma ya Walimu na Wizara ya Elimu ili kuhakikisha sekta ya elimu nchini Trans Nzoia inaendeshwa kwa ufanisi.

"Ikiwa kuna masuala ya kuhudumu bila shaka tutayachukua na TSC ili kuhakikisha kuwa tumepata walimu wa kutosha," alisema.

“Kama ni suala la miundombinu tutaenda kufanya mawasiliano na Wizara ya Elimu na kuona jinsi gani tutashirikiana hata kuhakikisha tu tumepata madarasa.

 

 

 

View Comments