In Summary
  • Kulingana na duru za habari ni kuwa  msichana wa miaka 12 anasemekana kujiua kwa kutumia kamba za viatu
Image: HISANI

Siku ya Ijumaa asubuhi, mtoto wa miaka 12 alijiua ndani ya nyumba baada ya mamake kumwambia kuwa yeye si mtoto wake,Eldoret kaunti ya Uasin Gichu.

Kulingana na duru za habari ni kuwa  msichana wa miaka 12 anasemekana kujiua kwa kutumia kamba za viatu.

Wakazi wamesema mtoto huyo alikuwa akipitia hali ngumu.

Mtoto huyo aliripotiwa kupata mateso mengi kabla ya kuamua kukatisha maisha yake nyumbani kwao huko Eldoret alikokuwa akiishi na nyanyake.

Bibi yake ameambia polisi kuwa mjukuu wake alitaka kwenda Huruma kaunti ya Nairobi ambako mamake anakaa lakini mamake hamtaki.

Bibi alipomjulisha mama yake na akasema kwamba hapendi kumuona msichana huyo, marehemu alikasirika.

Msichana huyo alijitoa uhai wakati bibi yake alipoenda dukani.

Akizungumza na runinga ya Citizen Bibi huyo alisema;

"Mtoto huyo alianza kisirani wikendi iliyopita,nilipika chakula lakini hakukula,aliniambia kwamba wanamitandao wanamwambia kwamba ananuka,"Alieleza.

 

 

 

 

 

View Comments