In Summary

Bonga points huzawadiwa mteja alama 1 kila anapotumia shilingi kumi ya muda wa hewa na wateja wanweza kuipata muda wa hewa shilingi 3 kwa alama 10,muda wa hewa wa shilingi 8 kwa alama 25 au kununua data ya mtandao kutumia alama hizo.

Afisa mkuu mtendaji wa Safaricom Peter Ndegwa akizindua programu ya M-Pesa mnamo Juni 23, 2021.
Image: SAFARICOM

Watumizi wa Safaricom wanaochelewa kulipa deni la okoa jahazi sasa watalipa deni lao kiotomatiko iwapo watakuwa na bonga points.Hatua hii imechukuliwa na Safaricom ili kuhakikisha matumizi ya mabilioni ya bonga points na kuishusha thamani yake.

Hatua hiyo pia itatahakikisha kuwa wale wanaopitiza masiku za kulipa deni lao la okoa jahazi wamelipa kutolewa kwa bonga points ili kilipa deni.

Mwishoni mwa mwaka uliopita,Safaricom ilitangaza kuwa watu waliokuwa na bonga points watakatiziwa bonga points mwanzoni mwa mwaka wasipotumia na kwamba huduma hii itakuwa na muda wa kuisha kinyume na hapo awali ambapo bonga points haikuwa na muda wa kuisha.

Tangazo hilo lilizua hisia tofauti huku wateja wa Safaricom wakipinga na kulalamikia Safaricom kwa kuweka muda wa kuisha kwa bonga points hatua iliyoifanya Safaricom kufutilia mbali tangazo hilo.

View Comments