In Summary

•Naibu rais, Rigathi Gachagua alimpa Raila Odinga changamoto ya kuwashirikisha wanawe kwenye maandamano.

Winnie Odinga

Binti yake kinara wa Azimio, Raila Odinga, Winnie Odinga sasa amesema kuwa atashiriki katika maandamano ya siku ya Jumatatu tarehe ishirini kupinga uongozi wa serikali ya Rais Ruto.

Katika chapisho lake kwenye ukurasa wa Twitter, Winnie aliwaambia wakutane kwenye uwanja wa maandaano.

"Tukutane barabarani," alichapisha Odinga.

Winnie Odinga aliteuliwa kuwa mbunge wa EALA mwaka wa 2022.

Winnie Odinga amekuwa kwenye mstari wa mbele kuunga mkono ajenda za baba yake ambaye ni kiongozi wa Azimio,Raila Odinga. Alimuunga mkono babake wakati wa kampeni ya kinyang'anyiro cha kiti cha urais.

Viongozi wengi  akiwemo naibu rais,Rigathi Gachagua walioshutumu maandamano iliyopangwa na Odinga walimwambia awahusishe wanawe wawe kwenye mstari wa mbele wa maandamano.

Kiongozi wa Azimio tarehe 20 Jumatatu  alidai kuwaongoza wafuasi wake kupinga serikali ya William Ruto. Baadhi ya shughuli alizosema watafanya ni ikiwemo kuandamana hadi kwenye ikulu ya Nairobi.

Raila alilalamika kuwa Rais Ruto amefanya maisha ya Wakenya kuwa magumu zaidi kwa kuondoa ruzuku ya mafuta na vyakula na hivyo kufanya gharama ya maisha kupanda. Alidai pia kuwa sava za IEBC zifunguliwe ili kutathmini mshindi halali wa uchaguzi wa 2022.

Licha ya hayo, Rais Ruto alipuuza madai ya Odinga akisema  anachotafuta ni kumhadaa na handsheki ingine ila ataambulia patupu, hata hivyo, Ruto alidai kuwa yuko tayari kushiriki na kiongozi yeyote yule kwa ajili ya amani na maendeleo na mustakabali wa nchi.

View Comments